Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

CRISTIANO Ronaldo amemgalagaza mpinzani wake Lionel Messi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 600 kwenye ngazi ya klabu baada ya kupasia nyavu katika mechi ya sare iliyopata Juventus kwa Inter Milan juzi Jumamosi.
 
Fowadi huyo, CR7 mwenye umri wa miaka 34, alifunga bao lake la 27 kwenye kikosi cha Juventus msimu huu na hivyo kumfanya awe amefikisha mabao 600 katika soka la klabu huku mpinzani wake, Messi akiwa amefunga mabao 598.
 
Ronaldo alifunga mabao 450 kwenye kikosi cha Real Madrid, ikiwamo zaidi ya mabao 50 aliyofunga kwa misimu sita mfululizo, huku kwenye kikoso cha Manchester United alikowahi kucheza, alifunga mabao 118.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…