Deportivo (Robo fainali, 2003/04)
Kipindi hicho, Deportivo La Coruna ilipokuwa kwenye ubora wake, robo fainali moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2003/04 iliwakutanisha wao na AC Milan. Kipindi hicho Milan nao walikuwa moto kwelikweli na mchezo wa kwanza uliopigwa San Siro, walishinda 4-1 na kuonekana kama wanatinga nusu fainali. Lakini, kilichowapata huko Hispania ni aibu, walipigwa 4-0, shukrani kwa mabao ya Walter Pandiani, Juan Carlos Valeron, Alberto Luque na Fran Gonzalez