MAAJABU yapo asikwambie mtu. Liverpool usiku wa juzi Jumanne walithibitisha hilo pale walipogeuza matokeo ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kisha kwenda kushinda 4-0 uwanjani Anfield kwenye mechi ya maruduano.
Ulikuwa usiku wa aina yake huko Anfield umeleta maana kwamba Barcelona sasa imekubali kupoteza vita kwenye mechi za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili mfululizo licha ya kufunga mabao yanayoanzia matatu katika mechi za kwanza.
Hata hivyo, hilo lililofanywa na Liverpool ni mwendelezo tu wa matokeo ya ajabu ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu kupindua matokeo baada ya kupoteza mechi za kwanza.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.