Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tony Adams : "Arsenal only lost once in 1991, I was in Chelmsford prison, I didn't lose that one.." Tony Adams defends his defensive record at Arsenal [BTsport score]

The 1990–91 season was the 93rd season of competitive football played by Arsenal.
Arsenal finished the season as league champions for the second time in three seasons, losing just one of their 38 league games.
mhhhhh tokea timu zinavaa boxer za kulalia
1095765
 
Kuna haka kajitabu kama mtazamo kama wako yani kinapinga kila adhabu inayosemekana Mungu atatupa ikiwepo kuchomwa moto kwamba Mungu hawezi kua katili kiasi hivyo....

View attachment 1095749

Kiumweli kuna vitu unaweza kuhisi haviko sawa lakini ndio hivyo tumewekewa mipaka sana.

Pole kwa kuumwa Macho mkuu
Kucha ileeeee
 
Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au hubadilika. Moja kati ya mambo ambayo hutokea ni mabadiliko kwa watu wanao mzunguka mtu huyo. Wengine humpenda, wengine humheshimu, wengine humchukia au hata kumwonea wivu.
 
Hawastaajabishwi na mafanikio ya wengine

Moja kati ya tabia kubwa ya watu wenye wivu ni kutostaajabishwa na mafanikio ya wengine. Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu.
 
Unaweza kusikia hata wakisema kauli kama vile “mbona hayo mambo ya kawaida”, “mbona wapo wengi waliofikia hapo”, “mambo ya kupita hayo, cha muhimu uzima bwana”, “mafanikio ya watu hayanihusu bwana”, n.k. Watu wenye tabia kama hii ni wakuepukwa maishani kwani wivu umewatawala.
 
Huhusianisha mafanikio na bahati

Watu wenye wivu huamini kuwa hakuna mtu mwingine anayestahili au mwenye uwezo wa kufanikiwa. Wao hujiona kuwa wao ndiyo wenye tiketi ya mafanikio na endapo basi yatatokea kwa watu wengine itakuwa ni kwa bahati tu.

Unaweza kusikia wakisema kauli kama vile, “hiyo kazi kaipata kwa bahati tu bwana”, “amepata dili kweli”, n.k.
 
Watu hawa, wengi wao huwa na wivu ndiyo maana hutaka yale yanayotokea kwa wengine yatokee na kwao. Utashangaa kuwaona mara unapofanya hiki nao wameshaiga, unapopanga hiki nao wameshaiga, unapoeleza umefanikisha hiki nao wanaeleza walivyokifanikisha tena hata kwa namna ambayo inaonekana inakuzidi.

Watu wa aina hii ni wenye wivu na watakunyonya nguvu ikiwa utashiriki kwenye mashindano yao.
 
Hupenda kuleta taarifa mbaya

Kuna watu ambao kila mara wao ni kuleta taarifa mbaya hasa juu ya jitihada zako za kimaendeleo au dhidi ya malengo yako.

Unaweza kusikia watu hawa wakisema kauli kama vile, “Aaa! yule jamaa mwenye biashara kama yako amefilisika”, “Inavyoonekana biashara kama hii yako huko tunakoenda haitakuwa na dili”, “ufugaji haulipi”, “biashara hazilipi”, “hakuna maana kuwekeza kwenye kilimo kwa sababu ni pata potea”, n.k.
 
Tabia hii ni ya watu wenye wivu wakitaka tu kukurudisha nyuma ili ukate tamaa na uwe na hofu ya kutimiza malengo yako.

Sanjari na hilo, watu wenye wivu hupenda kuzungumzia zaidi kushindwa kuliko kushinda. Wao watakueleza zaidi jinsi utakavyoshindwa kwenye kila unalolifanya kuliko utakavyofanikiwa.
 
Hufurahia wengine wanaposhindwa

Ukiona mtu anayefurahia kushindwa au kuanguka kwa mwingine basi ujue kiwango chake cha wivu ni kikubwa sana. Watu wasio na wivu husikitika pale wengine wanapoanguka; pia huwatia moyo ili wainuke tena na si kufurahia.

Kwa kuwa watu wenye wivu huwa hawapendi kuona meli ya mtu mwingine baharini, basi wao hufurahia sana mara wengine waangukapo au wapatapo matatizo.
 
Hawajumuiki pamoja kusherehekea mafanikio

Mtu mwenye wivu hapendi kuona mwingine akifanikiwa kumzidi yeye; hivyo itakuwa ni vigumu sana kwake kushiriki katika tukio lolote ambalo ni lakusheherekea mafanikio ya mtu mwingine.

Watu hawa huishia kutoa udhuru na vijisababu ambavyo vitawafanya wasihudhurie kwenye tukio hilo.
 
Hukusema vibaya kwa wengine

Je umeshaona watu ambao mkiwa pamoja wanakuwa marafiki wakubwa sana lakini ukiwapa tu kisogo wanakuwa nyoka wenye sumu kali? Kama jibu ni ndiyo, basi hawa ni moja kati ya watu wenye wivu.

Kiuhalisia tunao marafiki, ndugu, wafanyakazi wenzetu au hata majirani wengi wa aina hii.

Huja kwako kwa uso wa urafiki na wema lakini wakiondoka tu wanaanza kukusema vibaya ili kuharibu mahusiano yako na watu au kukwamisha kile unachokifanya.
 
Back
Top Bottom