Wakati wataalamu wa masuala ya lishe wakisisitiza ulaji wa vyakula tofauti ili kuupa mwili virutubisho vyote muhimu, kila tunda lina mchango mkubwa mwilini mwaka.
Mtaalamu wa lishe kutoka kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Elizabeth Lyimo anasema jamii inapaswa kufahamu kuwa ndimu na limau ni matunda yenye vitamini C ambayo husaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma.
Kwa mantiki hiyo matumizi ya ndimu na limau ni kichocheo kimajawapo cha kuongeza damu mwilini na wala si kupunguza kama watu wanavyodhani,” anasema Elizabeth.
Elizabeth anaasa ifahamike kwamba ndimu na limao husaidia kuongeza hamu ya kula hasa kwa mtu anayepata kichefuchefu na kutapika hivyo ulaji wa mara kwa mara wa matunda haya unakusaidia kukupa kichocheo ambacho kitasiaida kuongeza damu mwilini.
Mtaalamu huyo anasisitiza kuwa ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula mchanganyiko ili kupata virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwani hakuna chakula kimoja kinachotosheleza mahitaji yote ya mwili.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.