Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gorofa linauzwa
FB_IMG_1558296851673.jpeg
 
1102807

kwa mara nyengine Mzee amekosa uweledi na hekima ya kuzungumza, Mzaha kwenye dini tena mwezi huu wa swaum ni ukosefu wa nadharia ya kufahamu uzito wa shughuli yenyewe kwa waumin.
Anaposema kachanganyikiwa na sauti ya Qarii wa Quran wa kike ni dalili tosha kuwa hakustahiki kuwa sehemu ya mualiko wa tafrija hii adhim ya maneno ya Mwenyezi Mungu kwa waumin wa kiislam.
Mashindano haya si ya mzaha kama mpira bali ibada iliohitaji mwenye ufaham na uelewa mpana wa tafrija hizi za kiimani na umuhimu wake kwa jamii..
waandaaji wana mengi ya kusoma katika hili
 
Njaa imemtoa mafichoni, baada kumpigania Lowassa kwa miaka mitano sasa hana lake tena.
Ameona heri abanane kugombea teuzi za mzee baba
 
Mfano hadithi ya wazee waliokuwa wakifagilishwa barabara kwa matiti huko nyuma. Basi umuulize urefu wa hayo matiti hata yawe fagio yakifika magotini? Utakiona cha mtema kuni, wewe nani hata uwe na mantik ya kudadisi hadithi nadhifu ya rawahu yeye mwenyewe?
 
Iweje wewe udadisi haki ya ubora wa maisha kuliko poyoyo aliehangaika na akafika?
Ndio ukakuta mathalan unaweza kuwa na mtaa wa Mwenyekiti poyoyo wenye kisima cha maji na mashine ya kusukuma maji kijiji kizima lakini poyoyo akaizima isitumike kabisa kwa sababu itachakaa na kuharibika.
 
Mtazame Al-Bashir, kweli wa kufikwa na zahma ile katika umri huu?
Hivi kweli watateseka wakiuacha ufalme na uungu mtu wakiwa wastaafu waliojiimarisha kwa miaka na dahr?
Hivi hawasomi kwa wengine?
Itazame AU unafikiri nini kama si upoyoyo unaotuangusha?
 
Upoyoyo ndio uliolipelekea bara la Afrika likawa masikini kwa wananchi wake lakini tajiri kwa neema lilizojaaliwa zikawafaidisha wengine.
Upoyoyo ndio uliokuza utumwa, naam kwani hujui machifu wetu wenyewe walitajirika kukamata na kuuza wasiowapenda miongoni mwa wananchi wao?
 
Upoyoyo ndio ulioleta ukoloni na leo hii ukoloni mamboleo unakuzwa zaidi na upoyoyo wa “system” zetu. Itazame Afrika Kusini na mauaji ya waafrika kwa waafrika halafu fikiri tatizo ni kitu gani kama si upoyoyo uliorithishwa na kukuzwa katika vichwa vyetu wenyewe? Ah masikini! Wema walio wengi wamefunikwa na mapoyoyo wachache wenye nguvu na sauti inayokatisha tamaa ya ustaarabu mwema.
 
Poyoyo ni jeuri alieshiba kibri kwa sababu nae kapita katika mashaakil ya maisha magumu huko nyuma. Lazima nae akuadhib wakati mwengine kwa kufikiri adhab anayokupa ndio itakayokujenga kama ilivyomjenga yeye. Haki kwake yeye ni ya nguvu na ashki yake inavyompelekesha.
 
Back
Top Bottom