Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji16][emoji16]
Screenshot_20190520-112527.jpg
 
Mfumo wetu ndio wenye kulea haya yaliopo na ndio maana rasimu ya Warioba ikaweka uzito wa kimfumo kiasi kwamba hautegemei mkuu ni nani bali uhuru wa haki na uadilifu uliotukuka. Miaka minne hii na bado watu wanakula na hawanawi mikono. Umepata kuenda shughulini ukakaa na watu wanaonawa mikono yote miwili wakisubiri dhifa ipitishwe? Ndio yaliopo katika ripoti ya CAG.
 
Sifahamu hasa kelele za watukufu kumlaani mmoja aliesimama kidete katika ukweli na kufichua maovu yanayotendeka. Hebu itazame ripoti nzima kweli utalihakiki vipi na kulirekebisha neno DHAIFU kwa mazingira haya na ushahidi wa mambo yanavyokwenda?
 
la kujifunza kwa wengi tu ni kuwa si kukunja uso na kujibu kwa hasira na hamaki ndio ukaweza kusimamia haki. Katika lafdhi nzuri na za unyenyekevu ni za Profesa Assad. Kazungumza kwa maneno mazito na ya mvuto wa kumsikiliza bila ya kejeli, matusi, amri, majivuno na kukirihisha. Lakini uzito wake ni kama tetemeko la ardhi au Tsunami kwa jinsi lilivyopokewa.
 
#Sarafu

Turudi kutazama historia na jinsi gani haya masuala ya exchange rate yalipoanzia duniani. Baada ya vita ya pili ya dunia, Madeni yalitawala soko la dunia. Muingereza alidaiwa na Marekani, nayo ikiwadai Ufaransa na nchi nyengine zilizowasaidia katika vita ile; nao halkadhalika wakalielekeza deni kwa Ujarumani.
 
Inasemekana haya madeni yalianzia tokea vita ya kwanza ya dunia ila sasa hali ikawa mbaya zaidi katika uchumi wa dunia. Katika kulipana ndio likazuka hili suala la sarafu ya kulipana na kila mmoja akashashua thamani ya sarafu yake kama njia za kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na madeni yaliowazunguka
 
Back
Top Bottom