Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jibu ni kuwa ya sehemu yenyewe ina changamoto ya kimazingira na kuwafanya wakaazi wake wabebe azma ya kuhama mara kwa mara.
Wanasema wanahistoria kuwa huko nyuma kwa vile Hadhramut ni mfano wa bonde (Valley) kubwa, hufikwa na mafuriko ya mara kwa mara na kuna kipindi huko nyuma nusu ya wakaazi wake walipoteza maisha.
Mafuriko kama haya hasa miaka ya nyuma huzaa muda mrefu wa ugumu wa maisha maana watu hupoteza mfumo mzima wa kuishi na ndio sababu inayoeleza tabia za wahdharami kuwa wahamiaji kufuata mema kwengine (Pastures Green).
 
Nimekutana na mmoja wa wahusika kabisa wa huu mseto na msambwija ninaotaka kuueleza na uzuri wa Zanzibar katika mchanganyiko huu. Yeye ni mzanzibari kwa kuzaliwa lakini anabeba historia ya wazee wake moja kwa moja kutoka Hadhramut. Anapoizungumza historia hii mwili unaweza kukusisimka kwa jinsi ya uzuri wa visiwa hivi vilivyovutia wahamiaji wa asili tafauti huko nyuma.
Babu yake ni mhadhrami alieahama Yemen kuelekea visiwa vya Bali, Indonesia. Akaishi huko mpaka zilipoanza zahma za mifarakano na ukuaji wa vyama vya kikomonist. Wakahama wengi wao kurejea makwao kuepukana na migogoro hio.
 
Wengi wa wahadhrami wameenea kwenye mwambao wa bahari ya Hindi, wakiwa sehemu ya jamii ya wahamiaji nchini Singapore, Malaysia, India, na hapa Afrika Mashariki. Diaspora yao ni kubwa na ya kupigiwa mfano katika tafiti nyingi za mchango wa diaspora kwa nchi wanazotoka.
 
Safari ya kutoka Bali mpaka Yemen kwa majahazi ilikuwa ya miezi mingi, bahati mbaya wanafika Yemen wakakutana na yale yale waliyoyakimbia Bali na hivyo wakaamua kuelekea Zanzibar famili nzima kama sehemu mbadala ya kutazama muelekeo wa maisha yao mapya. Wakati huo kwa simulizi za wazee wake, Zanzibar ni Dubai ya dunia hii ya leo. Jahazi yao ikawaleta mpaka Somali, hapo haikuweza kuendelea tena na safari kutokana na uchakavu na urefu wa safari.

Babu yake alikuwa tayari ana mke wa Indonesia aliehama nae pamoja na watoto wake ambae anakuwa ni baba wa huyu mhusika mkuu; nae pia aliozwa mke wa asili ya Bali. Tayari lugha mbili zinazungumzwa hapo, kiarabu cha Yemen na kiindonesia katika familia moja.
 
Wakiwa kismayuu, Somali wakapoteza baadhi ya wanafamilia, kwa hio kuna makaburi ya watu wake wa karibu waliozikwa pale na kuwa sehemu ya mwanzo ya makaazi ya muda mfupi katika safari ya maisha mapya.

Pale wakasaidiwa jahazi nyengine ilioweta Zanzibar na walipofika wakapokelewa na familia za Hadhrami zilizokuwa wenyeji visiwani hasa mitaa ya Malindi.

Famili hizi zilikuwa na uwezo mkubwa na hazikuwaacha watu wake bure, waliwapokea na kuwatafutia makaazi na hata kazi ili waanze maisha yao mapya katika Zanzibar ya wakati huo. Majina ya familia hizi yapo na maaruf katika viunga vya Malindi, Zanzibar.
 
Wengi wao baada ya kufika visiwani wakatafutiwa nyumba mitaa ya Kikwajuni. Na hata taswira zao hubeba ule uchina uchina wa asili ya Bali na sehemu nyengine Indonesia huku majina yao yakiendeleza urithi wa asili za Yemen walipotokea. Jamii ya wahadhrami hawa ilikuwa kubwa Malindi na huku Kikwajuni kiasi kwamba waliozeshana wenyewe na wakaendeleza urithi wao wakiarab na Mashariki ya mbali.

Wengi wao walihama visiwani baada ya Mapinduzi na inasemekana meli ya mwisho iliokuja kuwachukua ilikuwa ya wadachi mwaka 1968 ambayo kwa huyu mhusika takriban mashangazi, wajomba, ami zake wengi waliamua kuondoka ila baba yake alibaki na kukataa katakata kurejea akikumbuka zahma za nyuma na sababu za kuhama familia nzima.
 
Leo hii kuna wajukuu na vitukuu vyake wenye nasaba ya Zanzibar na asli ya mchanganyiko. Na ndio sawa sawa na wale machina tambi wa Malindi, mabohora wa mji mkongwe, makumbaro, wangazija, washirazi, waomani na makabila tafauti yaliopo hapa, washihiri wa Yemen, wamakonde, wanyamwezi, wazaramo, wanyasa, wazulu (utafiti unahitajika zaidi) na wengi wa watu wetu ambao sote hubeba jina la Zanzibar kama ardhi mama iliotukutanisha pamoja kwa uzawa kwa sababu ya uhamiaji wa wazee wetu waliokaribishwa na wenyeji wakati huo.
 
Desturi ya uovu ni kuhakikisha victim anageuzwa kuwa ndie adui wa kushambuliwa na kudhalilishwa. Case study nzuri ni ya Lisu. Hakukutwa na ajali bali jaribio la mukusudi dhidi ya maisha yake, kapona kwa miujiza tu ya Muumba wake, anaeleza ubaya aliotendewa, wametoka wenye imani thabit wakimdhihaki, kumsuta na kumdhalilisha.
 
BBC HARD TALK
Lisu kapewa jukwaa zima la kujibu hoja za watawala akiwa victim alienusurika kifo cha ajab na mwenye lengo la kuomba ridhaa ya urais kipindi kinachofuata. Ni wachache sana wanaoshiriki vipindi vile kwa sababu ya mfumo wake unaobeba zaidi “Statesmanship” na “Prestige” ya coverage yake.

Yaani ni kama “Cross Examination” ya mdai mahakamani anavyopigwa masuala na team ya watetezi kuhakikisha ile “Beyond any reasonable doubt” inatimia. Huwezi kushiriki kipindi kile ukiwa kichwa kitupu kama daemusin
 
.
msamaha wa deni la umeme
  1. Hatukusamehewa ila tumeshinda hoja.
  2. Deni la VAT lililofutwa ni dogo mno kuliko miaka ya nyuma ambapo VAT hio ililipwa kwa mara mbili mbili kuliko sehemu yeyote ya mipaka yetu.
  3. Wakati umefika pia kutazama VAT kwa mafuta na gesi na “surcharges” nyengine hasa ile ya dola 10 ya storage wakati majirani zetu wao hulipa dola tatu.
  4. Wanaoshangiria hili ni wale wale waliowatusi waliokuwa wakilipigia kelele.
 
Unaweza kuwa na nchi masikini yenye ustaarabu na khulka njema. Umasikini wa aina hii huwa ni wa kipato, Lakini wananchi huonekana na aina ya furaha kwa sababu ya ukinaifu unaotokana na khulka na zile silka za unadhif, ihsan na kutosheka. Umasikini tulionao Barani Afrika ni umasikini si wa kiuchumi pekee bali wa khulka pia. Mfumo umejengeka kiubabe na kuzaa uovu na uonevu.
 
Matokeo yake ni anguko la akhlaq na mfumo mzima wa ustaarabu kama wanaadam wenye akili na maarifa. Na hakuna umasikini mbaya kama huu unaobeba anguko la khulka. Ungeliweza kurejesha kabisa khulka njema kabla ya kuuondosha umasikini. Baya zaidi ni kuwa hata ukianza kutajirika kama nchi isio na akhlaq basi maendeleo yake huwa tegemezi na si ya muda mrefu.
 
akili za wanachama na viongozi wa ccm.

Misamiati miwili bora kabisa kuwa shahidi wa haya yaliopo. Kwanza “Samaki” kwa maana ya usahaulifu wa kupita kiasi.Amani karume ambaye ndiye Aliewaita samaki hakukurupuka, wala hakuwatusi bali ni ushahidi wa hali ya sahau ya ajabu walio nayo.

Kujitekenya ukacheka mwenyewe nao ni msamiti thabit wa tamthilia tulio nayo. Unaunda tatizo mwenyewe, unalaumu mwenyewe, na unalitatua mwenyewe huku ukitaka hongera, makofi na vigelegele. Kujitekenya na kucheka mwenyewe ni maradhi yanayonasabishwa na upungufu wa akili. Sawa na usamaki na usahau wa kupindukia, vyote ni sehemu ya mapungufu ya utendaji mzuri wa akili na athari zake.
 
muungano wetu:
Unajuwa petrol inapoagizwa kutoka nje na kufika Bara huuzwa kwa wadau tafauti tukiwamo zenji. Lakini basi tozo ya uhifadhi wake kwetu ni dola kumi kwa kiwango cha ujazo maalum wakati nchi majirani hulipa chini ya nusu ya pesa hizo kwa ujazo huo huo? Kiurahisi watu milioni moja visiwani wanachangia mara tatu katika hizi tozo tu ndogo ndogo zilizowekwa. Hapo hujatazama VAT, faida ya kibiashara na hizo “service charges” kweli maisha yatakuwa na unafuu?
 
Demokrasia ni sehemu ya kipimo cha utu. Maendeleo yanawezekana yasiwe na maana ikiwa utu, haki na democracy haipo. Mfano mzuri Afrika Kusini wakati wa Apartheid, kimaendeleo sifikirii kama kulikuwa na nchi ya kiafrika iliokuwa mbele yake. Na vikwazo vyote walivyowekewa na dunia bado ilibeba ukubwa wa uchumi na maendeleo yake. Lakini hayakuwa maendeleo ya maana kwa sababu ya udhaifu mkubwa katika usawa, haki, heshima na utu. Maendeleo ya kweli ni yake yatayobeba uchumi bora sambamba na mfumo wa haki ilio thabit.
 
Sifahamu sababu ya Mwalimu kututoa katika mfumo wa demokrasia ya kibunge na kutupeleka katika mfumo dhaifu huu wa kiurais (Empirical Presidency). Sijui tuseme ni suala la wakati kama taifa changa au azma nyengine ya kuongoza katika misingi ya utukufu wa Rais kama chifu au mfalme. Hebu fikiri kama leo mjomba wake BAK angekuwa anajiwakilisha bungeni mwenyewe kujibu Bunge katika demokrasia ya kibunge angeliweza kuiepuka kura ya kukosa imani?
 
Utukufu wa nchi unabebwa na mamlaka ya Bunge na uhuru wa mahakama. Rais kama mkuu wa nchi anatakiwa abebwe na heshima ya bunge; bila ya imani thabit ya wabunge walio wengi basi hakutakuwa na uongozi thabit wa kidemokrasia. Na hivyo ni suala la lazima kuwa na bunge huru linalobeba mhimili wa nchi kwa umakini bila ya muhali, uchama na upendeleo. Hili limejengewa misingi madhubuti katika rasimu ya Kamati ya Warioba. JK angelijijengea heshima ya ajabu kama angeliliendesha kwa insaf zoezi zima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…