Nigendako
JF-Expert Member
- Dec 1, 2017
- 23,296
- 122,446
Poa bwana jezi(teena naona umeweka kwa avatar kabisa)Ha ha ha
Mambo Prisca?mambo yanaenda huko?
🙌🙌🙌🙌SIFA ZA MWANAUME ASIYE NA HELA:
1. Viatu huisha upande mmoja
2. Kushabikia YANGA
3. Hunywea maji kwenye jagi hata kama kuna glass au kikombe
4. Kupenda kuvaa suruali zenye rangi ya kung'aa.
5. Kufungua soda kwa meno
6. Kuvaa socks hadi magotini hata kama hayupo mazoezini
7. Anapenda sana kuangalia movie zilizotafsiriwa
8. Kufuta jasho kwa vidole
9. Kupiga miayo hadi machozi yanamtoka.
10. Kuingilia ugomvi hata wa watoto wadogo
11. Kumchukia kila mwanamke anayemiliki gari
12.Kumiliki smartphone iliyopasuka kioo.
13.Akitengewa chakula lazima amalizie kunywa mpaka na mchuzi kwenye kibakuli.
14.Kila mwanamke anayemchangamkia kwake anajua ashapata zari la kupendwa.
15.Wanapenda sana kutafuna vitumbua asubuhi asubuhi bila chai.
16.Akiingia kuoga bafuni, anahakikisha anasugua mpaka ndala akiamini usafi huficha umasikini.
17.Akipanda dala dala lazima ashike nauli mkononi ili isije kudondoka.
18.Wanapendaga sana kukaa siti za dirishani kwenye safari yoyote.
19.Ukiangalia mashati yake mengi utakuta kola za mashati zimeanza kuchanika. [emoji2088][emoji2088][emoji2088]
@BAK unaitwa huku[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
SASA IZO NI SIFA ZA WANAUME WASIOKUWA NA HELA AU NI SIFA ZA WANAUME NA WANAWAKE WANAOTOKA VIJIJINI AMBAKO BADO WANAAMINI MAGUFULI NA BAK HAWANA UHUSIANO WOWOTE WA KINDUGU
[emoji470] [emoji470] [emoji470]
SIFA 8 ZINANIHUSU HAPO JUU.
zisizonihusu
Sishabikii yanga wala timu yoyote Tanzania[emoji1022][emoji1022] sina meno ya kufungulia soda wala sina hela ya kununua soda zanzibar wapishi wa vitumbua ni wachache mnoo labda ukimbilie soko la mwanakerekwe ukutane na mama ntilie kutoka Bara, asubuhi nikiamka nakimbilia bakuli la urojo kama mbuzi mtoto anavyokimbilia maziwa sina stori na mwanamke kwa sababu ni mfuasi wa imani ya buddha simchukii mwanamke ila tukikutana namuangalia miguu yake, kama miguu yako ni mibaya kama ya ndovu a.k.a tembo hata salamu yangu sikupi, kwangu mimi uzuri wa mwanamke ni miguu na sio sura kama wanavyoamini wengineo sijawahi kula shughulini, nyumbani kwa mtu au mghahawani, lakini ninapokula nyumbani mpaka sahani nairamba kama mnyama paka[emoji250][emoji250] nikikuta watu wanapigana natafuta njia ya nyumbani ilipo, sipendi ujinga kwa sababu marehemu karume aliwahi kusema wanaume hawapigani ovyo ndio maana alipiga marufuku mchezo wa boxing suruali zangu zote nyeusi kwa sababu ni mvivu wa kuosha nguo na hata shuka langu jeusi. nikiingia chooni naosha mwili wangu kwa dakika tano tu halafu natoka mbio kama niliyefumaniwa, naziogopa sana sabuni za kunukia. Tafadhali usiniulize kwa sababu gani, nadhani jasusi BAK atakuwa na majibu. muda wote natembea na ndara huku kwetu zenji tunaziita kandambili, huo muda wa kuvaa soksi nitapata wapi? kiingereza sijui lakini nakaa na kamusi la oxford pindi ninapoangalia drama.
Ha ha ha umeanza na mambo yako ya jeziPoa bwana jezi(teena naona umeweka kwa avatar kabisa)
Mambo yanaenda kijela jela (lazima kumiliki laini ta titisielo)