Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hahahaha comment zako burudani tosha
 
NI hivi, Manchester United imeweka wazi kwamba itakwenda moja kwa moja kwa kiungo Tanguy Ndombele kama supastaa wake, Paul Pogba ataamua kuchukua virago vyake na kuihama Old Trafford.
 
Pogba, aliyenaswa kwa Pauni 89 milioni amekuwa haeleweki kwenye kikosi hicho akidai kwamba ndoto zake ni kwenda Real Madrid jambo linalomfanya Kocha Ole Gunnar Solskjaer kushindwa kufanya mipango yake kwa wakati.
 
Lakini staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameambiwa kama anataka kutua Bernabeu basi ni lazima aandike maombi ya kutaka kuondoka huku Man United ikiweka wazi mpango wake wa kwenda kumsajili Ndombele.
 
Man United inataka kusajili kiungo kuziba pengo la Ander Herrera, lakini kuhusu Ndombele itakuwa kwenye vita kali dhidi ya Paris Saint-Germain na vigogo wengine kama Real Madrid ambao wanavutiwa na huduma ya staa huyo wa Ligue 1.
 
Kiungo Toni Kroos amesema hatishwi na ujio wa Paul Pogba katika kikosi cha Real Madrid.
Kauli ya Kroos imekuja huku kukiwa na presha kubwa ya Pogba kujiunga na klabu hiyo katika usajili wa majira ya kiangazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…