Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kawaida uwanja huu, hutumiwa na vijana wa mtukutu Diego Simeone, naizungumzia Atletico Madrid, lakini safasi hii, nyasi zake zitanyanyaswa na miguu ya vijana wa Mauricio Pochettino dhidi ya Jurgen Klopp na wanae. Patachimbika unaambiwa!
 
Kwanini? hii itakuwa mara ya pili mfululizo kwa Liverpool wenye historia kubwa na michuano hiyo, kucheza fainali huku ikiwa ni fainali ya kwanza kwa vijana wa Mauricio Pochettino, tangu kuanzishwa kwa klabu ya Tottenham Hotspurs, miaka 136 iliyopita.
 
Wakati Wanda Metropolitano ukiruhusu watu 67,829 tu, kwengineko duniani, ikiwemo Tanzania tutapata fursa ya kushuhudia aidha ubabe wa Liverpool kwenye mashindano miongoni mwa vilabu vya England au rekodi mpya ikiwekwa katika historia ya Spurs, kupitia runinga zetu na mabanda umiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…