Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

July 31, 1964, Reeves na mshirika mwenzake wa kibiashara, Meneja Dean Manuel waliondoka Batesville, Arkansas kupitia Nashville wakitumia ndege ya injini moja akiwa Reeves anaendesha. Wawili hao walikuwa wamepata ‘dili’ ya kununua shamba huko Deadwood Texas, Kaskazini mwa Galloway ambayo ni sehemu aliyozaliwa Reeves.
 
Kutokana na watu walioiona ajali hiyo jinsi ndege ilivyoanguka na maelezo yaliyomo kwenye tape iliyorekodi mwenendo wa ndege, na pia maelezo ya ripoti ya ajali, kwamba Reeves alikata kushoto katika jitihada zake za kuipata Franklin road, ili afike uwanja wa ndege aweze kutua.
 
Reeves alitegemea zaidi hisia zake katika kumuongoza na hakutumia maarifa aliyofundishwa chuoni kuikabili hali kama hiyo. Baada ya masaa 42 mabaki ya ndege yalionekana ikiwa mbele, yaani usoni pamoja na injini vimejikita ardhini. Reeves na mwenzake walikutwa tayari wamekwisha fariki.
 
Tangu kipindi cha kifo cha Jim Reeves kulipotokea, Mary alipatwa na matatizo ya kuugua kabla hayajamzidia. Mjane huyo Mary Reeves alifariki akiwa na umri wa miaka 70, Novemba 11, 1999. Iliripotiwa kuwa alikufa akiwa peke yake katika nyumba ya kuuguza wagonjwa.
 
Kabla ya kifo chake Mary Reeves Davis alishindwa kusimamia mali za Jim kutokana na ugonjwa, zikauzwa kwa ‘United Show of America’ mwaka 1997 kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 7.3 Jim Reeves aliwekwa kwenye kundi la mwimbaji nyota wa kiume ambaye ametokeza katika midundo ya ‘Nashville Sound’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…