Mei 26 2018: Finali ya Champions League - Real Madrid 3-1 Liverpool, Olympic Stadium, Kiev
Gareth Bale alifunga moja ya bao kali zaidi katika soka ya Ulaya huku kipa wa Liverpool Loris Karius ambaye alimsababishia pigo Klopp pigo la kupoteza taji kuu nyingine kwa mara ya sita
The Reds tayari walikuwa wanakosa huduma ya mshambuliaji Mohamed Salah walipambana kiasi cha haja ambapo Sadio Mane alifunga bao la kusawazisha.
Lakini Bale aliingia na kufunga cao lingine la kushangaza kabla ya kuongeza lingine lililoipatia ushindi Real.
Mpango wetu ulikuwa kucheza na kushinda na wala sio lingine," alisema Klopp, amabye baadae alimtuma Kipa Karius kwenda Besiktas ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili.
Miezi 12 baadae, na baada ya kutolewa tonge mdomoni na Manchester City katika kinyang'anyiro cha fainali ya ligi ya Premier, Liverpool wanarejea tena kuasaka Ubingwa wa Ulaya kufuatia nusu fainali ya kusisimua dhidi ya Barcelona na kutinga fainali.
Je Klopp atavunjw amkosi wa kushindwa katika fainali... au atakubali kushindwa kwa mara ya saba mfululizo?
Beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 33, anasema kuwa Hazard ataisaidia sana timu hiyo ya Bernabeu iwapo atahamia klabu hiyo msimu huu. (Star)
Manchester United wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa PSG na Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 Adrien Rabiot, ambaye atakuwa ajenti huru kuanzia Julai mosi. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester United itamruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku kujiunga na Inter Milan msimu huu lakini iwapo klabu hiyo itamnunua kwa dau la £80m. (Times - subscription required)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Itali Andrea Pirlo anasema kuwa alikataa uhamisho wa kuelekea Manchester City 2011, huku Chelsea ikiamua kutomsajili 2009 kwa sababu ya umri wake. (Mail)
Arsenal inamtaka winga wa Bournemouth na Uskochi Ryan Fraser, 25, lakini matumaini yao ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, yamedidimia baada ya kushindwa kufuzu katika kombe la mabingwa Ulaya. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, beki Shkodran Mustafi, 27, na raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 30, huenda ni miongoni mwa wachezaji watakaopigwa kalamu huku Arsenal ikitafuta fedha za kuimarisha kikosi chake.. (Star)
Mwenyekitiwa Liverpool Tom Werner amesema kuwa ni muhimu kwamba mkufunzi wa klabu hiyo Jurgen Klopp, ambaye amekuwa akiifunza timu hiyo tangu mwezi Oktoba 2015 anasalia katika klabu hiyo kwa muda anaotaka.. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 27, hajaamua kuhamia katika ligi ya Premia hatua itakayowacha klabu za Juventus na Napoli kushindania saini yake. (Marca)
Klabu mpya iliopandishwa daraja ili kushiriki katika mechi za Premia Aston Villa inataka ,kumsaini kiungo wa kati wa Bournemouth Harry Arter, 29, lakini huenda ikakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Fulham na Stoke katika kumsajili mchezaji huyo wa Ireland.. (Irish Independent)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kuifunza klabu ya Itali Roma (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Beki wa Ufaransa na Manchester City Eliaquim Mangala, 28, anatarajiwa kurudi katika klabu ya Porto - miaka mitano baada ya kuondoka ili kuhamia kwa dau la £32m. (O Jogo - in Portuguese)