Mkuu napata ulevi adimu kabisa kimya kimya nimeipiga mvulilizo
View attachment 1114428
mkuu nimecherewa kukijibu
hii
empress ki inanishinda kila ninapojaribu kuitazama, nimeishia episode ya 11 tokea miaka miwili iliopita.
kuna drama inaitwa
shin don ndio naifuatilia kidogo dogo pamoja na age of warriors hizi zote zinaizungumzia tawala ya goryeo a.k.a wang clan empire
shin don alikuwa ni monk nyakati za utawala wa goryeo chini ya mfalme gongmin kama nipo sahihi, alizaliwa na msichana aliyekuwa ni mtumwa na baba yake alitokea familia za mboga 300 lakini ndio hivyo nyakati hizo kuzaa na kijakazi ilikuwa ni laana kuliko kuhongwa IST.
nyakati hizo goryeo bado ilikuwa chini ya MONGOLIA kama tunavyofahamu mongolia waliikalia kimabavu goryeo kwa miaka 80.
huyu shin don alikuja akawa ni mwanadamu mwenye nguvu kubwa sana na aliyekuwa akiaminiwa na mfalme kuliko kiongozi yoyote.
historia inamzungumzia shin don kwa pande mbili
- muhubiri wa dini aliyekuwa na uchungu wa nchi yake kwa sababu alipopata nguvu alipambana sana na matajiri na wanasiasa waliokuwa wakiwaonea walala hoi, nyakati hizo walala hoi hawakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi na wao ndio walipaji kodi wakubwa kuliko matajiri.
- muhubiri aliyetumia mwamvuli wa dini kwa ajili ya kujitengenezea nguvu ndani ya nchi, inasemekana jamaa alitumia madaraka yake vibaya sana, ilifika nyakati kauli yake (madaladala) ilikuwa na nguvu zaidi kuliko kauli ya mfalme (jiwe)
ndani ya drama hii pia umezungumziwa uhusika wa empress ki pamoja na kaka zake, huyu mama wakorea wanamchukia sana kwa sababu alipoolewa na mfalme wa yuan mongolia alitumia vibaya madaraka, aliithamini zaidi nguo yake ya ndani (chupi) kuliko goryeo ambako ndiko alikotokea licha ya kwamba aliuzwa kama mtumwa.
ilifika nyakati goryeo aliiendesha kwa kauli zake si unajua tena alikuwa akipendwa sana na mtawala wa mongolia, ndipo akatumia nafasi hii kuwapa nguvu za kiuongozi kaka zake ndani ya serikali ya goryeo (pro mongolia)
ikazuka vita kati ya anti mongolia wakiongozwa na mfalme gongmin dhidi ya pro mongolia, baadae mongolia tawala yao ikafa ndipo ikazaliwa ming china.