Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Burudani zinaendelea
Screenshot_20190602-105633_Facebook.jpeg
 
Taarifa za kutoka Italia zinadai kwamba kila kitu kinaonekana kuwa wazi kabisa kwamba Sarri anaachana na Chelsea kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi hasa baada ya kuwapa ubingwa wa Europa League na kuwarudisha kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Anakwenda Juventus kuchukua mikoba ya Max Allegri, aliyefutwa kazi baada ya kuipa timu hiyo mataji manane mfululizo ya Serie A. Lakini, huko anakoondoka Chelsea, wenyewe wameweka orodha yao ya makocha wanaotajwa kwamba huenda wakaenda kuchukua kazi akiwamo kiungo wa zamani wa timu hiyo, Frank Lampard, ambaye kwa sasa ni kocha wa Derby.
 
Lampard amekuwa na msimu mmzuri huko Derby na jambo hilo ndilo linalowafanya wengi waamini kwamba anastahili kurudi kuinoa timu yake ya zamani. Makocha wengine wanaotajwa hapo ni Max Allegri, anayeoondoka Juventus, Patrick Vieira, Diego Simeone na Nuno Espirito Santo.
 
Chelsea inahitaji kuwa kwenye mikono ya kocha makini kutokana na ukweli kwamba msimu ujao watakuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa na zuio la kufanya usajili huku supastaa wao wa nguvu Eden Hazard akiripotiwa kuwa na mpango wa kuachana na timu hiyo akielezwa kutimkia zake Real Madrid.
 
Hata hivyo, mambo yote hayo hakuna kitakachotokea hadi hapo Sarri atakapoamua kuondoka. Kama akibaki basi hakuna kocha mwingine atakayekuja Stamford Bridge kwa sababu Chelsea wataendelea kubaki na huduma ya Mtaliano wao huyo.
 
Back
Top Bottom