Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alifunga bao pia kwenye ushindi wa 3-0 iliyoupata CSKA dhidi ya Real Madrid huko Bernabeu, hivyo Emery anaamini kuwa na huduma ya straika huyo haiwezi kuwa shida sana kama wakali wake Aubameyang na Lacazette wataondoka.
 
Kocha Emery angekuwa na pesa nyingi za kusajili, zaidi ya Pauni 100 milioni kama chama lake lingefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwe Chelsea kwenye fainali ya Europa League na kumaliza Ligi Kuu England nje ya Top 4 kimetibua mpango huo.
 
HOFU imeanza kutanda kwa watu wa Liverpool. Tahadhari imetolewa na mtu mmoja anayejua fitina za soka. Anaamini kwamba mastaa wao wawili, Sadio Mane na Mohamed Salah lazima watafuatwa na klabu mbili kongwe za Hispania, Barcelona na Real Madrid.
 
Liverpool walitwaa ubingwa wa Ulaya wikiendi iliyopita huku wakiukosa kidogo ubingwa wa England msimu uliosha na Mane na Salah wamekuwa na mchango mkubwa kikosini hapo huku wakitengeneza moja kati ya safu bora ya ushambuliaji Ulaya.
 
Real Madrid na Barcelona watakuwa wananusanusa kuhusu Salah na Mane na nadhani mmoja kati yao lazima atawindwa katika dirisha hili la uhamisho. Timu zote hizo mbili zipo katika mchakato wa kujijenga upya na wana uwezo wa kumnyemelea mchezaji yeyote wanayemtaka” alisema Souness.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…