Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. "Kuna wanaosema wamebakwa, kwani sisi (wanaume) ni wabakaji sana? Juzi kuna waliokamatwa Coco Beach hivi nao watasema walibakwa? Hizo NGO zianzishe shule za kusomesha hao wenye mimba sio serikali yangu."

2. "Ndio maana sisafiri ili niwanyooshe humu ndani kwanza. Leo nilitakiwa kuwa Ethiopia lakini nimemtuma Makamu"

3. "Kuna mtu hapa Sengerema amekula Bilioni 2 za maji, nawahakikishia kabla sijaondoka nitakua nimemjua"(hii ndio imeniacha hoi)

JPM 04/07/2017, Sengerema.!
 
Edson Jonasi Zvobgo (Waziri wa zamani wa Zimbabwe) aliwahi kusema bungeni "Mheshimiwa Spika nusu ya wabunge katika bunge hili ni wapumbavu". Wabunge wakalalamika wametukanwa. Spika akamtaka afute kauli yake na aondoe maneno yake maana ni ya kuudhi (yasiingie kwenye hansard).

Zvobgo akasimama na kusema "Mheshimiwa Spika nafuta kauli kwamba nusu ya wabunge ni wapumbavu, nirekebishe kauli hiyo kwa kusema kwamba nusu ya wabunge katika bunge hili si wapumbavu".

Wabunge wakapiga makofi "Pwapwapwa".!!
 
Back
Top Bottom