Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unabaki kumtazama tu Profesa Kabudi na kisha kutabasamu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚. Namkubali. Ni moja ya vichwa vinavyofanya kazi sana. Niliishia darasa la saba kwa hiyo awali sikupata nafasi ya kufundishwa naye, lakini waliowahi kufundishwa naye wanasema jamaa ni โ€˜kichwa sanaโ€™.
 
Kwa bahati, hatimaye sasa nimebahatika kufundishwa naye. Hiki anachoendelea kutufanyia ni fundisho tosha. Hata wanafunzi wake wa zamani kwa sasa nao tena darasani. Ametuingiza darasani katika somo linaloitwa โ€˜mabadiliko ya mwanadamuโ€™.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Edo wa Kumwembe mabadiliko kama ya huyu wengi tutayakataa.
 
Niliyemsikia na kumuelewa ni tofauti na huyu lakini hata hivyo hili ni sehemu ya somo kutoka kwake. Kwa mfano, sasa anatufundisha kwamba kumbe โ€˜uprofesaโ€™ bado ni jalala tu. Tulioishia darasa la saba tulidhani kwamba hii ni ngazi ya juu zaidi katika elimu. Kumbe hapana. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Profesa anaamini kwamba kabla ya kutinga geti la Ikulu kwenda kuapishwa alikuwa anaishi jalalani ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Kumbe hata wale waliobaki pale Mlimani na kwingineko wako jalalani. Wakati ule namuangalia kwa husuda kubwa pale Mlimani City akila โ€˜lunchโ€™ yake huku nikiwanongโ€™oneza wenzangu โ€˜Profesa Kabudi huyoโ€™ kumbe alikuwa jalalani? Kumbe alikuwa mavumbini? Nichukue fursa hii kumpa pole.
 
Siku moja akiachana na nafasi yake, zama zake zikiisha kule juu nadhani wanajalala wenzake watamkaribisha jalalani. Kwa sasa wamuache kidogo afunguliwe mlango wa V8. Mwanadamu anaishi mara moja tu. Nani anataka shida?
 
Profesa pia anatufundisha kwamba ndani ya mabadiliko ya mwanadamu unapaswa kuwa mpole. Ni kama alivyo sasa. Namba Moja ameweka wazi wakati mwingine huwa anamtukana Profesa tusi la chapchap ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚la โ€˜mpumbavuโ€™. Ni neno zito. Kama unabisha mwambie hivyo aliyekwambia kama atakubali.
 
Profesa akiambiwa hivyo anaendelea kuchapa kazi kwa nguvu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Maprofesa wa zamani wangefanya kile kitu kinachoitwa kulinda heshima binafsi. Kwa Kiingereza wasomi wakipita maskani kwetu huwa wanasema โ€˜to protect my dignityโ€™. Wale wa zamani huwa wanaachia ngazi na kurudi shule kufundisha.
 
Ni vema tukafahamu kwamba katika maisha rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi sana yakiwemo mambo ya kwenye mapenzi, biashara, kupata nafasi kazini, mahusiano na marafiki zenu au kwenye mikataba au tenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ