Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mastaa wa Ligi Kuu ya England Alexis Sanchez (£24m), Mesut Ozil (£24m) na Mo Salah (£20m) ni miongoni mwa wanamichezo walioingia katika orodha ya 100 bora wakati nyota wa Real Madrid, Gareth Bale anashika nafasi ya 79 baada ya kuingiza kiasi cha Pauni 21 milioni.
 
Serena Williams aliyeingiza Pauni 23 milioni anakuwa mwanamke aliyeingiza kiasi kikubwa zaidi kwa mwaka wa fedha ambapo hata hivyo alishika nafasi ya 63. Mwaka mmoja uliopita hakukuwa na mwanamke aliyejitokeza katika orodha ya 100 bora.
 
Bosi mkuu wa Jarida la Fobres, Kurt Badenhausen alisema: “Kutanuka kwa soka duniani kote kumeonekana wazi katika mapato mwaka 2019, huku mastaa watatu wa soka Messi, Ronaldo, na Neymar wakiongoza katika orodha.
 
Hata hivyo, kikapu kimeendelea kutawala katika 100 bora huku kukiwa na wanamichezo 35 ambao wameingiza kiasi cha Pauni 1 bilioni huku asilimia 72 ya kipato chao ikitokana na mishahara yao zaidi kuliko mikataba binafsi ya biashara.
 
Kulikuwa na nchi 25 zilizotoa wanamichezo hawa matajiri tofauti na mwaka 2018 ambako kulikuwa na wanamichezo 22. Marekani imetawala ikiwa na wanamichezo 62 wakati Uingereza ilikuwa na wawakilishi watano ambao ni Joshua, Hamilton, Conor McGregor (£37m), Rory McIlroy (£31m) na Justin Rose (£25m).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…