Mimi sijui nikoje naweza kumpenda mwanamke ila akinikubalia tukifika chumbani naona aibu kumchungulia
Yaani mwanamke akivua nguo zake mpaka ya ndani kabisa akabaki uchi wa mnyama Mimi huwa machozi yananitoka nalia halafu namuaga nakimbia. Sijui yale machozi yanatokaga wapi
Sio Mara moja au mbili huwa nawaacha wanawake wenyewe vyumbani
Yaani sijui kwanini naogopa uchi wa wanawake kama nini sijui.
Sasa mtoto mdogo ndio akitaka kukojoa karibu yangu huwa namfukuza kama mbwa au niondoke Mimi hata kama nipo ugenini
Hivi hii inasababishwa na nini?