Musoma huko kijijini kipindi fulani nilikuwa huko miaka ya hamsini hivi. Kibibi kiliichimba mkwara familia moja hivi korofi kuwa itapigwa na radi na kweli zikapita siku mbili radi ikapita ikaua ng'ombe kadhaa. Hiyo familia wakapuuzia mikwara ya kenyewe kakawaambia kuwa safari nyingine itakuja kali zaidi na kuleta uharibifu mkubwa zaidi. Hiyo familia walikuwa ndo wamenunua mashine ya kusaga na kujenga nyumba ya kisasa kubwa. Radi ikarudi ikapiga hiyo nyumba na mashine na vyote vikateketea. Bado hawakusarenda. Kakawaambia safari hii radi itakaporudi itaua watu. Wakajichanga wakaenda kuomba msamaha. Ikawa ndiyo pona yao. Sijui pengine ilikuwa ni coincidence tu au kulikuwa na namna. Haya mambo ni magumu...