Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Kevin De Bruyne– Pauni 117 milioni

Licha ya kwamba Manchester City iliweza kubeba taji la Ligi Kuu England bila ya huduma ya Kevin De Bruyne kwa sehemu kubwa ya msimu, lakini bado huko sokoni staa huyo wa Kibelgiji thamani yake bado ipo juu.
 
KDB ubora wa huduma yake ni kitu kisichokuwa na mashaka na ndio maana hata thamani yake huko sokoni imekuwa kubwa. Rekodi zinafichua hii leo ukitaka kumsajili staa huyo beki yake ni Pauni 117 milioni, ndivyo soko linavyofichua sokoni.
 
Raheem Sterling– Pauni 126 milioni

Staa mwingine wa Manchester City kwenye orodha hii ya wachezaji ambao bei zao sokoni zimechangamka. Raheem Sterling amekuwa na msimu mzuri kabisa huko Man City akiisaidia timu hiyo kubeba mataji yote matatu makubwa huko England, ikibeba Ligi Kuu England, Kombe la Ligi na Kombe la FA.

Wakati mwingine amekuwa akichaguliwa kuwa nahodha wa England.

Ubora wa huduma yake uwanjani, Sterling ukitaka kumnunua weka mezani Pauni 126 milioni.
 
Harry Kane– Pauni 135 milioni

Harry Kane amekuwa mtu muhimu wa kuipigia mabao Tottenham Hotspur na Timu ya Taifa ya England kwa miaka ya karibuni. Alishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia 2018 alipokutamba na kikosi cha England.

Alikuwa msimu mzuri pia huko Spurs kabla ya majeraha kumtibulia. Lakini, kwa sasa ukitaka huduma ya Kane atue kwenye kikosi chako, basi jipange na mkwanja unaoanzia Pauni 135 milioni kwa sababu ndiyo thamani yake halisi.
 
Mohamed Salah– Pauni 135 milioni

Liverpool ilimsajili Mohamed Salah kwa pesa isiyozidi Pauni 40 milioni akitokea AS Roma na tangu wakati huo amekuwa bonge la staa huko Anfield na kuonekana kwamba imefanya biashara ya maana.
 
Staa huyo ameshinda Viatu vya Dhahabu kwa misimu yote miwili aliyokipiga kwenye kikosi cha Liverpool na msimu uliopita aliisaidia timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa Transfermarkt, Salah anauzwa Pauni 135 milioni.
 
Timu Messi leo wako wapi? Cole Williams na King Davet njooni huku GOAT wenu anasemwa [emoji16][emoji16][emoji16]

Na Prisca njoo uchukue points zaidi za kuwa unatumia kumtetea CR7 wako [emoji16][emoji16][emoji16]

Hahahahaha
Hoja yao hiyo wanaipenda sana japo haina nguvu na msingi, huyo Messi ni bora kwenye kila idara,ni aina ya mtu ambaye yupo royal sana kwa watu wanaomthamini imagine

Tangia azaliwe na pesa zote anazolipwa kama mchezaji anaelipwa zaidi Duniani lakini ana mwanamke mmoja na hajawahi kuchepuka

Tangia aanze kucheza mpira senior level yupo timu moja Tu ambayo ni Barcelona yote kwa yote huwezi ukapenda au ukahama makusudi kutoka Masaki/Osterbay aende kuishi Tandale/Tandika

Hivi Leo uambiwe kuna uzi mwingine wa kupeana likes afu uhame uzi huu uende huko hii haiwezekani sababu uzi huu ni bora na ni mkubwa, huo mwingine utakuwa underdog

Au kwa wanavyofikiria, Messi Leo hii akihamia Psg, Juve, au Manchester city hatoweza kuchukua trophies, waseme Tu wana mahaba na Ronaldo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…