Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Juu ya hayo, kuna mengine aliyoyaandika yenye kushangaza. Mfano ni pale alipouliza ni nchi ngapi za “Afrika ya Kiarabu” zilizowahi kushiriki katika ukombozi wa nchi za Afrika bila uswahiba wa kidini? Kwa “Afrika ya Kiarabu” anakusudia mataifa ya Afrika ya Kaskazini.
Inaonyesha hajui mchango mkubwa wa Morocco, ilipokuwa chini ya utawala wa Mfalme Mohamed wa Tano na Mfalme Hassan wa Pili, babu na baba wa Mfalme Mohamed wa sasa, katika ukombozi wa Afrika. Chini ya tawala zao, Morocco ilivisaidia kwa hali na mali vyama vya ukombozi vya nchi kadhaa za Kiafrika, na si kwa sababu za kidini.
 
Hata vuguvugu la kupigania uhuru Kenya lilifadhiliwa kwa kiwango kikubwa na Morocco. Joseph Murumbi, Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya, kabla ya uhuru akisafiria pasi ya Morocco.

Babake Murumbi alikuwa Goa na mamake alikuwa Mmasai. Lakini wenzake kina Jomo Kenyatta hawakufikiri kuwa mchanganyiko wake wa damu ulimpunguzia Uafrika wake.

Nadhani hata Mihangwa asingemkatalia Uafrika wake; labda angeutilia shaka lau babake Murumbi angetokea Afrika ya Kaskazini au “Afrika ya Kiarabu,” kama aitavyo sehemu hiyo ya Afrika.
 
Au pengine angekereka lau babake Murumbi angekuwa Mjapani kwa sababu Mihangwa ameandika:
“Tanzania imo mbioni kuimarisha mizizi ya ulaghai huu kwa kukubali kuanzisha Uraia wa nchi mbili kwa wageni na kwa Watanzania. Kwa mtindo huo, hatutashangaa siku moja, kwa mfano, Bunge letu kuongozwa na Spika Mjapani.”
Kutakuwa na ubaya gani, au patatendeka dhambi gani, ikiwa patazuka Mtanzania mwenye asili ya Kijapani akaliongoza Bunge? Akitokea, tumpime kwa macho yake ya kubana au kwa uzalendo wake?
Inavyoonyesha Mihangwa angekereka lau Rais wa zamani wa Congo Joseph Kasavubu angelikuwa rais wa Tanzania.
 
Mimi ningekereka lakini kwa sababu za imani, za itikadi za siasa na sio kwa sababu za jinsi yake. Babu yake Kasavubu, mzaa babake,alikuwa Mchina.Hilo lingemtaabisha Mihangwa.
Pengine angelikuwa raia wa Gabon, Mihangwa angeanzisha kampeni ya kumpinga Jean Ping, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika, asiwe mgombea urais wa nchi hiyo.
1135156
Babake Ping alikuwa Mchina.Kwa hivyo, kwa mantiki ya Mihangwa, Jean Ping ni “Mwafrika bandia”.
Kadhalika Mihangwa ama hajui au amesahau mchango wa Algeria kwa ukombozi wa Afrika ya Kusini na nchi nyingine zilizokuwa bado zikitawaliwa na wakoloni baada ya Algeria kuwa huru.Na Algeria haikutoa msaada huo kwa sababu za kidini.
Wala Gamal Abdel Nasser aliyekuwa Rais wa Misri hakusaidia ukombozi wa nchi za Kiafrika kwa sababu za kidini.
 
Asingefanya hivyo kwa sababu nchini mwake kwenyewe akiwakandamiza wanaharakati wa Kiislamu wa kundi la “Ikhwan Muslimin”.
Mihangwa anaendelea kunishangaza anapozungumzia “utamaduni wa Kiafrika” kana kwamba Afrika ina utamaduni mmoja, hata katika hiyo anayoiita “Afrika Nyeusi”.

Afrika haina utamaduni mmoja; ni bara lenye tamaduni mbalimbali. Huenda baadhi yao zikawa zinafanana lakini huwezi kusema kwamba ni utamaduni mmoja.

Na sijui Mihangwa anamzungumzia Profesa Ali Mazrui yupi anapoandika kwamba Mazrui hakuwahi“kutoa mawazo ya kujenga kwa Bara la Afrika, mbali na kujishughulisha na siasa za migogoro ya kimataifa na mitafaruku ya kidini – kati ya Ukristo na Uislam.”
 
Pengine Mihangwa ameyasahau tu mengi ya Mazrui kama alivyosahau jinsi nchi za Kiafrika zilivyosimama kidete kuiunga mkono Libya wakati nchi hiyo ilipowekewa vikwazo na madola makuu. Kama hakusahau basi asingeliuliza: “Afrika nyeusi inajitoa mhanga vipi kwa ndugu zao wa “Afrika ya Kiarabu” wanapopata majanga, kuonesha kwamba Waafrika ni wamoja?”
 
Jengine alilolisahau Mihangwa ni kutwambia walikotokea Waberber, wenyeji asilia wa Afrika ya Kaskazini.
Historia inatwambia kwamba Waberber wamekuwa wakiishi Afrika ya Kaskazini miaka 10,000 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (Yesu Kristo).

Hii leo wametapakaa Algeria, Morocco, Tunisia, Libya, Mauritania, Mali na Niger. Na wapo hata Misri. Wengi wao wana rangi ya dhahabu. Nao pia ni “Waafrika bandia”?

Hii tabia ya Waafrika kubaguana wenyewe kwa wenyewe baina ya “wenye nchi” na “wananchi”; na baina ya Waafrika “wananchi” na Waafrika “wageni” ndiyo sababu kubwa ya Waafrika kufika hadi ya kuchinjana wenyewe kwa wenyewe Afrika ya Kusini.
 
Habari hizo ziliihusu serikali yao. Rais Julius Nyerere aliibadili serikali yake kwa kuliteua Baraza jipya la Mawaziri. Majina ya mawaziri na wizara zao zilipotangazwa, ilibainika kwamba baada ya miaka mingi Nyerere aliona bora abadili mtindo na awe na waziri kamili wa sheria.
 
Chaguo lake la waziri wa kuiongoza wizara mpya lilikuwa Julie Manning. Manning alikwishapata umaarufu kwa kuwa mwanamke pekee katika kundi la mwanzo la wanafunzi waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuingia chuoni humo 1963. Kadhalika, yeye ni mwanasheria wa kwanza wa kike na jaji wa kwanza wa kike nchini Tanzania.
 
Nyerere na Fundikira walitoka mbali. Wote walikuwa watoto wa machifu, waliosomea Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Muhimu zaidi walikuwa wapiganiaji uhuru wa Tanganyika. Juu ya yote hayo, miaka michache tu baada ya uhuru walikorofishana na mwaka 1963 Fundikira alijiuzulu uwaziri. Nyerere hakuona haja ya kumteua waziri mwingine wa sheria hadi 1975 alipomteua Manning.
 
Kipindi hicho kilikuwa kipindi kigumu kwa sheria na kwa haki za binadamu Tanzania, hasa Zanzibar ambayo ilikuwa na mfumo wake wenyewe wa kisheria uliokuwa wa ajabu ajabu. Huko, watu wengi walifungwa jela bila ya kushtakiwa.

Kuna waliokamatwa na vyombo vya dola na ambao hadi leo hawajulikani walipo na kuna walioteswa mateso ya kila aina hadi wakafariki. Kuna waliokamatwa kwa visingizio vya kisiasa na kuna waliokamatwa kwa sababu za wivu.
 
Back
Top Bottom