Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Padmore akatoa rai ya namna ya kulitanzua tatizo hilo.

“Tutauandika mwaliko kwa namna ambayo wakikubali kuja, mabwana zao wa kikoloni hawatokuwa tena na imani nao, na watajikuta peke yao,” alisema Padmore.

Taarifa ya mwaliko wa mkutano huo wa mwisho wa mwaka wa 1958 iliulaani vikali ukabila. Kwa vile ukabila ulikuwa moja ya nguzo za ASP, kama ilivyotazamiwa Karume aliupinga mkutano wa Accra.
Asante mkuu kwa nondo zako za leo. Nimejifunza mengi sana...
 
Ubaguzi ndio tishio kwa Umoja Afrika
Chanzo: Raia Mwema tarehe 22 Aprili 2015

WIKI iliyopita, Joseph Mihangwa,mwandishi mwenzangu wa Raia Mwema,aliandika makala gazetini humu chini ya kichwa cha maneno “Dini za kigeni ni tishio kwa Umoja Afrika.” Ni makala yasiyo na nia njema.Sifichi, binafsi yalinichafua.

Nilianza kuingia hasira lakini nikajirudi nikikumbuka kipande cha wimbo wa kale wa Pate kisemacho: “hasira hasara mno, mno hasarani.”
 
Makala hayo yalinichafua kwa sababu mbili. Moja ni kwamba kuna baadhi ya mambo yaliyoandikwa humo ambayo si sahihi. Si sahihi kihistoria wala si sahihi kimantiki.Kwa hakika, mna mahali ambamo Mihangwa ameinyonganyonga mantiki utadhania anainyonga shingo ya kuku.
 
Sababu ya pili ni usafihi ambao Mihangwa ameunyunyiza hapa na pale katika makala mazima. Kwa mfano, kuna pahala ameandika: “Siku zote popo si wa kutegemewa; kwani utii na uaminifu wake hautabiriki.”Kwa ufupi, popo haaminiki.
Ni maneno mazito hayo.

Mazito kwa sababu “popo”anayemzungumza ni mwenyeji wa Afrika ya Kaskazini. Unaweza kuirefusha maana yake ya “popo” kuwa ni Mwafrika aliyechanganya damu au aliye na utamaduni wa Kiarabu na unaweza kuirefusha zaidi maana yake ya “popo” kuwa ni Mwafrika aliye Mwislamu.

Hoja kama hizi za “kipopo” lazima tuzipopoe kwani ni za hatari. Ni hoja za kibaguzi, za chuki, zinazoweza mara moja, kama kufumba na kufumbua, ikazusha balaa kama tunalolishuhudia siku mbili hizi Afrika ya Kusini.
 
Msamiati wa “Afrika nyeusi”, anaoutumia Mihangwa, ni msamiati wa ukoloni mamboleo unaopendwa kutumiwa na wale wanaochochea mgawanyiko wa Afrika.
Ni sawa na lugha waliyokuwa wakiitumia ilipokuwako Sudan moja. Wakisema “Waislamu wa Kaskazini na Wakristo wa Kusini” au “Waarabu wa Kaskazini na Waafrika wa Kusini.”
Msamiati huo ulitumiwa kupalilia moto uliowashwa kwa kuni nyingine lakini ulisaidia kutimiza lengo la kuigawa Sudan na kuikata pande mbili. Matokeo yaliyokusudiwa tunayashuhudia.
 
Nililikuna bongo langu kwa muda mrefu nikijiuliza iwapo niyagusie machache kati ya aliyoyaandika Mihangwa au niyapuuze yote. Waarabu wana usemi wao: “Jawab safih, skut.” Yaani jawabu ya safihi ni kumkalia kimya. Kumwacha na yake na kuuacha usafihi wake umzongereshe mwenyewe.

Baada ya kutafakari nikaona si uungwana kufanya hivyo kwani Mihangwa ni mmoja wa waandishi wa Tanzania ninaowastahi. Kwa hivyo, badala ya kumpuuza ni kheri kumkosoa. Aidha, si busara kuuacha upotoshaji wake utubabaishe Waafrika, hususan vijana wetu.
Ndipo nilipoamua kwamba ku-“skut” sito-“skut”. Nitaandika. Sitostaajabu ikiwa, kwa kuunukuu huo usemi wa Kiarabu, nimewaudhi wenye chuki na “Uarabu” au chochote chenye kuhusika na utamaduni wa Kiarabu au Uislamu, barani Afrika.
 
baadhi ya nyakati mpaka inafikia hatua unahoji maamuzi ya mungu kwa nini alimuumba mamba?
hawapi wenzake raha wanapokuwa na hamu ya maji, cha ajabu yeye muda wote yupo majini wala hakerwi?
mamba ana wivu wa kipumbavu kuliko baradhuli (gay) anapomuoena wivu mwanamke kupewa matiti na sehemu ya mbele ya siri.
Mkuu [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hoja alizozitoa Mihangwa wiki iliyopita alikwishazitoa mwaka 2010 katika Raia Mwema (toleo la 122). Hakufanya vibaya kuzikariri. Alipoteleza ni kuushadidia upotoshaji wa historia.
Nionavyo, kwa muhtasari, asemacho Mihangwa ni kwamba mtu hawezi kuwa Mwafrika, mwenye hisia za Kiafrika, ila awe mweusi. Kwetu Zanzibar, fikra kama hizo tunaziita fikra za “ugozi,” na za ubaguzi usio na haya. Zimechangia sana kutufanya tusiendelee.

Miongoni mwa maswali yanayomwenda akilini mwake Mihangwa ni: “ni nani anayeweza kuitwa Mwafrika wa kweli? Ni ipi Afrika ya kweli na Waafrika wa kweli?”
Jibu la kizalendo ni kwamba hakuna “Afrika ya kweli” na “Afrika danganyifu.” Iliyopo ni Afrika moja na tunataka tuzidi kuijenga iwe na umoja wa kweli, umoja wa kisiasa.
 
Afrika ya “ugozi”, Afrika aitakayo Mihangwa haipo. Haijawahi kuwako na wala haitakuwapo. Bara la Afrika daima limekuwa bara la mchanganyiko. Huo ndio utamu wake, ndio haiba yake na hatimaye mchanganyiko huo ndio utaokuwa nguvu yake.
Uafrika si rangi. Uafrika, hasa katika enzi hizi za utandawazi au utandaridhi, ni imani.
 
Ndiyo maana Afrika daima itawalaani mahaini wake akina Moise Tshombe aliyekuwa mweusi kama makaa na itaendelea kuwaenzi wazalendo wa Kiafrika kama akina Pio Gama Pinto wa Kenya aliyekuwa na asili ya kutoka Goa au mpigania uhuru wa Zanzibar, Ruti Bulsara, aliyekuwa na jadi ya Kiparisi kutokea India au Joe Slovo wa Afrika ya Kusini aliyekuwa Kamanda wa Umkhonto we Sizwe, lililokuwa Jeshi la Ukombozi la chama cha ANC.
Slovo aliyekuwa na asili ya Kiyahudi alizaliwa Lithuania na alihamia Afrika ya Kusini pamoja na wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka minane.
 
Sijui Mihangwa atawaweka wapi wananchi wa Cape Verde ambao wengi wao ni machotara au makrioli, yaani watu waliochanganya damu.

Na machotara wa Cape Verde wamechanganya damu chungu nzima. Wazungu wa mwanzo kuishi huko walikuwa mabaharia wa Kihispania na wa Kitaliana. Wakafuatiwa na walowezi wa Kireno. Baadhi ya Wareno hao walikuwa Waislamu na wengine walikuwa Mayahudi.
Wote walifululizia kwenda kuishi Cape Verde wakikimbia mateso ya Mahakama ya Kanisa Katoliki dhidi ya waumini wa dini za Kiislamu na Kiyahudi hasa katika karne za 15 na 16.
 
Damu nyingine za wananchi wa Cape Verde ni za Waholanzi, Wafaransa, Waingereza, Waarabu (kutoka Lebanon na Morocco), Wachina (hasa kutoka Macau), Wahindi, Waindonesia, za Wamarekani, damu za Wabrazil (wenye asili za Kireno na Kiafrika) na damu za watu kutoka nchi nyingine za Amerika ya Kusini.
Yapo baadhi ya mambo aliyoyaandika Mihangwa ambayo ni sahihi na hayapingiki. Mfano kwamba Waethiopia na Wamisri wa kale walikuwa watu weusi.
 
Back
Top Bottom