Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UNAWEZA UKAWA UNAMPENDA SANA ASIKUPENDE,FANYA UAMUZI SAHIHI.

UHUSIANO wenye amani na masikilizano ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu anakihitaji na ikiwa hivyo unaweza ukajikuta unanawiri tu!
 
Wakati mwingine unaweza hata kujikuta hujala chochote lakini ukajihisi umeshiba eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa naye karibu tu, yaani yeye kwako ndiyo mambo yote, yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha yako! Huo ndiyo utamu wa maisha!
 
Lakini sasa wakati wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wengine wanaoishi na wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa, yaani hawana furaha kabisa!
 
Screenshot_2019-06-25 Instagram(1).png
 
Kwao kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao licha ya kwamba wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote. Cha ajabu sasa, licha ya baadhi ya watu kutokuwa na furaha katika maisha yao ya kimapenzi eti wanahisi njia sahihi ni kuvumilia huku wakiamini siku moja mambo yatabadilika.
 
Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati. Mapenzi, nijuavyo mimi ni kupenda, kupendwa, kusikilizana, kupatilizwa na kuheshimiana na si kinyume chake! Wakati mwingine unaweza kujikuta katika wakati mgumu wa kuamua hatima ya uhusiano wako na mpenzio kwa kuwa unahisi unampenda sana na kwamba hauko tayari kumkosa.
 
Back
Top Bottom