Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati. Mapenzi, nijuavyo mimi ni kupenda, kupendwa, kusikilizana, kupatilizwa na kuheshimiana na si kinyume chake! Wakati mwingine unaweza kujikuta katika wakati mgumu wa kuamua hatima ya uhusiano wako na mpenzio kwa kuwa unahisi unampenda sana na kwamba hauko tayari kumkosa.