Kutambuliwa huko kulipata nguvu baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, Bwana Glanville, alipomueleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Count Herbert von Bismarck, kwamba Uingereza inatambua maeneo hayo ya Ujerumani katika bara ya Afrika Mashariki. Wakati Tanganyika inaanza kuchorwa na Wajerumani, Zanzibar tayari ilikuwa na mikataba ya kibalozi na Marekani, Uingereza, Italia, Ufaransa na Ubelgiji. Takriban nchi zote hizo zilikuwa na balozi zao Zanzibar. Marekani, kwa mfano, chini ya Balozi wao ambaye alikuwa pia alikuwa mfanyabiashara, Bwana Richard Waters, ilikuwa ikifanya biashara kubwa na Zanzibar wakati huo.