UNAAMBIWA hivi, ukichoka watu wanakuchoka zaidi. Hicho ndicho kinachomtokea beki wa kati Shkodran Mustafi huko Arsenal, kwamba timu yake kwa sasa inataka kumuuza hata kwa bei ya kutupa.
Arsenal wamepoteza matumaini kwenye beki wao huyo wa Kijerumani baada ya msimu uliopita kufanya makosa mengi yaliyowagharimu hasa kwenye mechi za mwisho za msimu.
Alisababisha penalti za kizembe sana kwenye mechi za sare dhidi ya Crystal Palace na Tottenham Hotspur kabla ya kwenda kufanya makosa mengi kwenye mechi ya kipigo cha nyumbani Emirates mbele ya Palace.
Taarifa za kuhusu staa huyo zilielezwa: “Baada ya fainali ya Europa League, Unai Emery ambaye siku zote alikuwa na imani na Mustafi licha ya kufanya makosa mengi, ameona inatosha. Hataki tena abaki hapo, anachotaka auzwe tu.
Arsenal sasa inafukuzia huduma ya mabeki William Saliba na Kieran Tierney huku Mustafi akiwa kwenye rada za AC Milan, ambapo Arsenal wanapiga sala usiku na mchana ili Wataliano hao waje kumchukua aondoke kwenye timu yao.
ARSENAL itapaswa kuchagua moja kusuka au kunyoa. Ni hivi, wakali hao wa Emirates wanasaka huduma ya winga mmoja matata na mipango yao kwenye hilo ni kumsajili staa wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Zaha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.