Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika sayari yetu hii ya dunia ambayo ni ya tatu ktk mzunguko wa dunia kuna aina kuu mbili za maji,waani Maji baridi (fresh water) na Maji chumvi (Salt water),Zaidi ya asilimia 3% ya maji yote yaliyopo duniani ni maji Baridi wakati asilimia 97% ya maji ni maji chumvi.
 
64818425_354586741906951_5867675844302505263_n.jpg
 
Kuna mito mingi sana inayoapatikana sehemu mbalimbali ktk dunia,mito hii utaofautiana kwa vyanzo vyake,asili,ukubwa,uapana,urefu,kiwango cha maji kinachotiririsha,kina,aina za viumbe vinavyoishi na hali ya hewa ya maeneo ipiayo mito hiyo.
 
Mto Nile,Amazon,Mississipi,Congo river,YangTse,Mekong river ndio mito mirefu zaidi duniani na inasafirisha kiwango kikubwa zaidi cha Maji kwa sekunde na hatimaye kwa mwaka,mito mingi inamwaga maji yake ktk bahari zaidi kuliko sehemu nyingine.
 
Mto Nile unaopatikana Barani afrika ndio mto mrefu zaidi duniani ukianzia Ziwa victoria afrika mashariki na hatimaye kuishia nchini Misri kaskazini mwa afrika ukiwa na urefu wa kilomita 6,853 km ukipitia nchi za Uganda,Ethiopia,Sudan na nyinginezo.
 
kukujulisha machache sana juu ya mto AMAZON ambao ni wa pili kwa urefu Duniani ukiwa na urefu wa kilomita 6,992 km ukiwa umeanzia ktk Milima ya Andes inayopatikana ktk Bara la Marekani ya Kusini,sehemu kubwa ya mto huu iko ktk nchi ya Brazil amabyo ndio kubwa zaidi barni humo.
 
Chanzo kikuu cha mto huu kinajulikana kama MUNTARO ktk milima ya Andes,lakini hata hivyo mto huu mrefu unapita ktk nchi za Venezuela,Bolivia,Colombia,Ecuador,Peru na hatimaye Brazili na kumwaga maji yake ktk bahari ya Atlantiki.
 
Mto huu moja ya faida yake kubwa unapita ktk miji mikubwa ya bara hilo la marekani ya kusini zaidi ya miji 13 mikubwa,watu wengi wa miji hii wanautumia mto huu ktk shughuli nnyingi ikiwemo kilimo,ufugaji,usafiri,viwandani,matumizi ya maji nyumbani,uvuvi na utalii ktk pori kubwa linalofahamika kama Amazon Jungle.
 
Back
Top Bottom