Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zaha ameripotiwa kuwa chaguo la kwanza la kocha Unai Emery katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini tatizo ni kwamba bajeti yake ya usajili ni Pauni 45 milioni.
 
Nyakati zile enzi Ujerumani imegawanyika, kulikuwa na ukuta mkubwa wa Berlin unaozitenganisha Ujeremami Mashariki na Ujerumani Magharibi.

Siku moja baadhi ya watu wa Ujerumani Mashariki walijaza gari taka lenye kila aina ya uchafu na kuutupia upande wa pili wa ukuta.

Watu wa Ujerumani Magharibi wangeweza kuwarudishia kwa kutupa uchafu upande wa pili tena hata zaidi. Kilichowashangaza wengi ni kuwa badala ya kurejesha matakataka wao waliamua kutuma *madikodiko* kama vile mikate, maziwa, nyama za kopo na mazagazaga kibao kisha wakayaweka kwenye package safi na kuyaweka upande wa pili. Lakini juu ya mzigo waliouweka upande wa pili wakaandika bango kubwa linalosomeka:

*"KILA MMOJA HUTOA ALICHONACHO"*

Maneno haya sio tu yaliwaumiza waliotupa matakataka bali yaliwafanya wajione hawafai kwa kila kitu. Ilikuwa ni kisasi cha akili.

Jiulize, Je, wewe una nini ndani yako?

Upendo au Chuki?
Vurugu au Amani?
Uhai au Umauti?
Uwezo WA kujenga ama Kubomoa?

Je, Umejifunza nini? *"KILA MMOJA HUTOA ALICHONACHO"* Fikiria, Jifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…