Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

$$£&(yaani poti huyu huyu ninae mjua mimi?!! Ina maana ankoo wangu binti mpole 'kanigwa' ngwala kihisia na mpori mpori?!!... Iti kanti bi) $$$View attachment 1152850

Yaani wewe kila sehemu lazima unitilie kauzibe. Pale kwenye tuition Mtendeni ukanizibia kwa Semeni, hapa tena unataka kuleta zako. Safari hii lazima nikushushe mnyama tu! [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Wakati technolojia imesababisha vitu vingi kuwa rahisi maishani mwetu, kuchagua jokofu zuri miongoni mwa zaidi ya mamia ya aina za majokofu sio rahisi kama ambavyo wengi wanafikiri. Aina ya maisha na ukubwa au udogo wa familia ni baadhi ya mambo yanayoathiri aina ya jokofu unalotakiwa kuwa nalo.
 
Hatua ya kwanza kabisa itakayoamua aina ya jokofu unalolitaka ni kiasi cha pesa ulichotenga au ulichonacho. Kama ilivyo kwa bidhaa zingine, majokofu yanapatikana katika bei tofauti tofauti kulingana na uzuri, ukubwa au udogo, ama hata kampuni iliyotengeneza jokofu hilo.
 
Utahitaji kujua upana na urefu (width and height) wa jokofu unalotaka kununua. Kwa ujumla hata kama utahifadhi vyakula na vinywaji vingi(ikiwa tu ni kwa matumizi ya nyumbani) utahitaji jokofu lenye urefu na upana usiozidi 1.7m urefu na 0.9m upana yaani 170cm(68inches)urefu na 90cm(36inches).
 
Jokofu lako jipya litahitaji kukaa vizuri katika jiko lako ama sehemu nyingine yoyote utakayoona inafaa. Hivyo kuwa makini unapopima ukubwa wake, bila kusahau kupima urefu na upana wa milango na njia litakapopitishwa jokofu wakati wa kuingia ndani.
 
Chagua aina kadhaa tofauti tofauti za majokofu. Kila moja likiwa na faida/uzuri (pros) na hasara/ubaya(cons) wake. Angalia bei,aina na mwonekano wake. Tafakari mwenyewe ikiwa unahitaji jokofu la milango miwili au mmoja, au ikiwa unataka lile linalopooza upande wa chini na upande wa juu linagandisha kabisa na kinyume chake. Au wakati mwingine unataka linalopooza upande wa kushoto na kugandisha upande wa kulia.
 
Angalia namna jokofu lilivyo kwa ndani. Chunguza kama lina vyumba ambavyo ni adjustable kwa maana ya kuweza kuongeza au kupunguza urefu wa vyumba vilivyomo(shelves that split) kulingana na mahitaji yako ya wakati husika. Majokofu mengine yana vyumba ndani yake visivyoweza kupunguza au kuongeza urefu (height) wake.
 
Angalia aina ya jina la kampuni ambalo ikitokea limeharibika basi ni rahisi kupata mafundi na vipuli vyake kwa ajili ya matengenezo. Jaribu pia kuuliza kutoka kwa watu wengine unaowafahamu kuhusu aina ya jina la kampuni la jokofu unalotaka kununua ikiwa wana uelewa au wameshawahi kutumia au wanatumia aina ya jokofu unalolitaka.
 
Ni vizuri pia kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kutoka kwa mtaalam yeyote unayemwamini ambaye ana leseni inayotambuliwa na serikali. Ni muhimu sana kufanya hivyo kwani kuna mambo mengine mengi ya kitaalam yanayopaswa kuzingatiwa ambayo hayawezi kuandikwa humu na kila mtu akayaelewa.
 
Katika hali ya kawaida kabisa sitegemei mtu atamtafuta fundi umeme inapotokea taa imeungua katika chumba, ofisi au nyumba yake. Kwa yeyote yule, taa isipowaka jambo la kwanza atakalofikiri ni taa kuungua. Mara nyingi ukweli huwa ni huo isipokuwa labda kama imetokea ni idadi fulani ya taa haziwaki na kwamba tatizo hili limeanza kwa muda mmoja basi huwa kuna sababu zingine za kiufundi. Nataka kutoa ushauri kwako kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia unapoamua kununua bulb mpya.
 
Kutokana na ongezeko la aina tofauti tofauti ya taa zinazotumia umeme, ni ukweli kwamba kumetokea machaguo mengi ya kutosha ya taa hizi. Ni vizuri ukazijua aina mbalimbali ya taa zinazotumia umeme kidogo. Pamoja na kuwepo aina nyingi sana ya bulb, leo ntaongelea aina mbili tu ambazo ndizo za kileo na zinatumia umeme kidogo kama ambavyo umeziona katika picha hapo juu mapema. Kuna Compact Fluorescent Light(CFL) ambazo wengi tumezoea kuziita Energy Savor na Light Emitting Diode(LED) ambazo kwa hapa Tanzania wengi huzitumia sana katika umeme wa mfumo jua (Solar Power) na kwenye Tochi nyingi sana za siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…