Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kikokotozi (calculator)

Ikiwa unataka kufanya mahesabu kadhaa, huhitaji kikokotozi au simu yenye kikokotozi kama uko karibu na Google. Kwa kuandika neno calculator kwenye ukurasa wa Google mara moja utapata kikokotozi kwa ajili ya kufanyia hesabu.
 
Kufahamu muda wa jua kuchomoza na kuzama

Kupitia Google unaweza kutazama muda wa kuchomoza na kuzama kwa jua kwenye eneo fulani.

Kwa mfano unaweza kuandika “sunrise Nairobi” au “Sunset Dar es Salaam” kwenye Google na utapata muda wa jua kuchomoza au kuzama kwenye mji husika.
 
Viwango vya kubadilisha fedha

Je umekuwa ukipata shida kufahamu viwango vya kubadilisha fedha mbalimbali duniani?

Usihangaike tena, unaweza kuandika “currency convertor” kwenye Google na mara moja utapata ukurasa kwa ajili ya kufahamu viwango vya kubadilishia fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…