Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bro bhana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We unaona ni sawa bro? Ni mtego utakaoangamiza marijali wengi sana hasa ukizingatia kwamba hata kuangalia kwa kutamani tu tayari moto unakuhusu....
 
Kivipi kutokuonesha likes kunaweza kuwakwamisha wanaoendesha maisha yao huko IG bro?
Advertisers wanaangalia wingi wa likes na comment ili kujua kama akaunti ina followers ambao wako active; na hivyo wanatoa mkwanja bila wasiwasi huku wakijua kuwa mkwanja wao haupotei bure. Kuwa na followers wengi tu haisadii sana kama siyo active na wanaoona kulaiki na kucomment kwenye tangazo lililowekwa. Nimesikiliza mjadala mkali kwenye redio leo asubuhi...

LeMutuz kwa mfano alikuwa analalamikiwa kuwa pamoja na kuwa na followers karibia laki 7 lakini post zake zinakuwa na likes na comments chache sana. Hii inamaanisha ama followers wengi ni feki (bots) au hawako active jambo ambalo siyo zuri kwa advertisers.
 
Nikweli wanaangalia hivyo, me pia niliwaza hivi vitu ila nikajijibu kwamba itabidi muhusika ascreen shot likes zake mana kwake zitakua zinaonekana alafu awatumie wenye tangazo wajue wanamlipa kiasi gani
 
Aisee sikuwahi kujua kama wanalipa kwa style hii
 
Aisee,,kwenye hili ww unaona ni sawa bro?wakiondoa likes na comment hawata yumba kwa namna flani hv
Sehemu yeyote mabadiliko yanapotokea kuyumba hakuepukiki ila watu watazoea, unajua kuna watu hawapo huru na IG kutokana na idadi ndogo ya likes wanayopata inawafanya kujisikia inferior, sasa kwa hili nao watakua huru....

Kuhusu Comments kama unavyojua malalamiko hasa mastar wakilalamika kila siku kutupiwa maneno machafu sasa hii itasaidia sana kupunguza hivi vilio
 
Kwani IG wenyewe walianzisha hii kitu wakijua watu watafanya biashara au watu wenyewe ndio walijiongeza tu? Kama wahusika halikua lengo lao sidhani kama watazingatia sana hivi vilio
 
Ngoja tusubiri bro,nafikiri kwa sababu hii ya Kanye na kama kweli IG watalifanyia kazi bhasi kuna idada ya mastaa wataongezeka na hata wasio mastaa kujiunga na IG!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…