Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inatajwa kuwa chanzo kimojawapo kikubwa cha inferiority complex, msongo wa mawazo na hata kujiua. Ni tatizo kubwa ndiyo maana hatua hii inaungwa mkono sana na wanasaikolojia wengi.
 
Kwani IG wenyewe walianzisha hii kitu wakijua watu watafanya biashara au watu wenyewe ndio walijiongeza tu? Kama wahusika halikua lengo lao sidhani kama watazingatia sana hivi vilio
Hapana. Mabadiliko (hata ambayo hayakukusudiwa) yanapojitokeza na kuathiri huduma yako inabidi uyazingatie. Hawa jamaa wana followers mamilioni na ndiyo hasa wanaisukuma IG kubakia kileleni. Huwezi tu kuwatupilia mbali. Youtube wamepelekwa mahakamani kutokana na tabia yao ya kufungia channel za watu bila huruma hata kama mtu anategemea channel hiyo kuendeshea maisha yake. Na watetezi wa haki za binadamu na masuala ya ajira wanasema wataishia kulipa mamilioni ya dola. Youtube wamesema wataunda timu itakayokuwa inapokea malalamiko ya watu waliofungiwa akaunti zao na kuyashughulikia kihalali. Platforms hizi zinaendeshwa na watumiaji; na watumiaji wana haki pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…