Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukute nae marehemu alikuwa na kibri kwa mume na dharau(sura nzuri +ghorofa) kwa majirani zake.
Hata kama umefanikiwa kimaisha lazima ujichanganye na majirani. Kitaani kwetu tunasema "kulipia mtaa kwa vijana" yaani baba mzima unajichanganya na vijana unapiga nao gambe, muda si muda wanaanza kupigana mkwara wenyewe kwa wenyewe "mtu asing'oe saiti mila wala fagio la bi mkubwa lisipotee hapa maskani... Abdul umeelewa?"
Laiti angekuwa anaishi nao vizuri, kabla moshi hauja panda kwa Mungu, masela wangekuwa wamemwagika na ndoo za maji....
 
Mkorea wa Zenj. Unasalimiwa na komando Jecha
bado sauti yake naendelea kuisikia kupitia masikio yangu dhaifu.

nimeamua kufuta uchaguzi kwa sababu tumegundua baadhi ya vituo hususani pemba kulifanyika udanganyifu, vile vile mgombea mmoja wa uraisi amejitangazia matokeo hivyo basi kwa mamlaka niliopewa natangaza marejeo ya uchaguzi yatafanyika machi 20.

kabla sauti ya jecha haijanguruma CCM walikuwa kimyaaaaaaaaa kama maji ya mtungini
babu shimba asikwambie mjinga yeyote hakuna utamu kama wa madaraka ya kulevya, mwanasiasa kukosa madaraka ni sawa na aliyefariki.

unabaki unajiwazia: akiingia madarakani mpinzani ile chain yangu ninayoitegemea kuwapa ajira jamaa zangu itazikwa rasmi.

ile chain yangu ninayoitumia kuwadhulumu wanakijiji ardhi zao ili nijenge hoteli za kifahari na majumba ya kuwahifadhia ndugu zetu kutoka BARA itazikwa rasmi.

ile chain yangu ninayoitumia kwa ajili ya kufanya biashara za magendo, biashara bila ya kodi zitazikwa rasmi.
 
Kuna maeneo ni upweke sana kigamboni sio kama kwetu Uswahilini Mbagara nyumba zimebanana mno.
 
Aiseee. Ndiyo maana watu hung'ang'aniamo na hata kujaribu kumshawishi mtu wao abadili katiba ili aendelee kubakia madarakani nao waendelee kufaudu. Mwalimu Nyerere aliwahi kulizungumzia hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…