Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1563475021026.jpeg
 
Swala la mtu wa kuoa au kuolewa naye ni swala nyeti linalohitaji maamuzi yanayohusisha hekima, utulivu, kumwomba Mungu pamoja na uchunguzi wa kutosha. Maisha ya watu wengi yamekuwa na matatizo makubwa kutokana na kufanya makosa katika kuchagua mtu wa kuoa au kuolewa naye
 
Ana malengo na maono

Hakikisha mtu unayetaka kuoana naye ni mtu mwenye malengo katika maisha yake. Mtu mwenye malengo hujishughulisha kila mara kuhakikisha anaandaa baadaye yake.

Mtu asiyekuwa na malengo huwaza matumizi na anasa kuliko kuzalisha; hafanyi kazi wala hajali kuhusu kesho. Hakika mtu kama huyu hawezi kuingia kwenye ndoa ikadumu au akaweza kulea familia yenye ustawi mzuri.
 
Anakuheshimu na kukuthamini

Heshima na kuthaminiana ni msingi muhimu katika ndoa. Nimeshuhudia mwanandoa akimzarau au hata kumbeza mwenzi wake mbele ya wageni au watoto; ni wazi kuwa tabia hii ilianza siku nyingi.

Ni muhimu kuhakikisha mtu unayetaka kuoana naye anathamini utu wako kuliko hata vitu vingine. Hakikisha anakusikiliza na kujali pia hisia zako.
 
Anajali na kuheshimu ndugu na familia yako

Ndoa ni kitu kinachounganisha watu wengi, watu wanapoingia kwenye ndoa familia mbili huungana kupitia ndoa hiyo.

Hivyo ni muhimu kuhakikisha mtu unayetaka kuoana nae anathamini na kuheshimu familia yako. Naamini usingependa mama, baba, shangazi, mjomba au ndugu yako wa damu adharauliwe na mwenzi wako.

Hivyo chunguza msimamo na tabia ya yule unayetaka kuoana naye ukoje juu ya familia yako kabla hamjaoana.
 
Anakuamini

Migogoro mingi kwenye ndoa inatokana na wanandoa kutokuaminiana. Kamwe usikubali kuoana na mtu ambaye hakuamini vyema.

Nimeshuhudia watu wakiwekewa watu wa kuwafuatilia, simu zao zikifuatiliwa na hata kuwekewa sheria kali kutokana na mwenzi mmoja kutokumwamini vyema mwenzake.

Kumbuka! Kama anakupenda kweli atakuamini na kuwa mwaminifu kwako.
 
Hakutamani bali anakupenda

Watu wengi hutamaniana badala ya kupendana. Tamaa huongozwa na vitu au mwonekano wa nje tu.

Hakikisha unaoana na mtu ambaye hata ukiwa mgonjwa, mzee, maskini au dhaifu bado atakupenda tu jinsi ulivyo. Kumbuka pia upendo wa kweli hautaki malipo wala hauulizi kwanini. Tamaa huhusisha hisia kali na baada ya muda hisia hizi hutoweka na kuisha kabisa ila upendo huhusisha bidii, kujitoa, kuvumilia na akili nyingi.
 
Anamheshimu Mungu

Watu wengi hupuuza nafasi ya Mungu katika mahusiano na maisha yao kwa ujumla. Ni muhimu ukakumbuka kuwa kwa asili binadamu hakuumbwa kukaa bila imani ya kitu chochote.

Mwenzi mwenye hofu ya Mungu atakujali, atakuheshimu, atakuthamini, atakutia moyo, atakuombea na hata kulea familia katika maadili mema.
 
Back
Top Bottom