Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1563474843263.jpeg
 
Anakufanya ufurahi

Kuna watu wanakaa kwenye mahusiano na watu ambao hawawapi furaha lakini bado wanaendelea kung’ang’ania hadi ndoa. Inawezekana hiii ni kutokana na upendo kujengwa kwenye vitu kama vile pesa n.k.

Kumbuka kuwa hakuna mbadala wa ndoa, ukishaingia umeingia; hivyo hakikisha mtu unayeoana nae anakufanya ufarahi kila mara na si uhuzunike maana utahuzunika maisha yako yote.
 
Anakusaidia kuwa bora zaidi

Je ulikua hujui kuvaa akakufundisha kuvaa? Ulikuwa hujui kupika akakufundisha kupika? Au umejifunza vitu vipya kutoka kwake?

Ni muhimu ukajiuliza maswali kama haya ili uweze kupata mwenzi wa maisha ambaye anaweza kukufanya kuwa bora zaidi na si kukurudisha nyuma au kukuacha ulivyo.
 
Ni msikivu

Usikivu ni tabia muhimu sana kwenye ndoa. Hakikisha yule unayetaka kuoana naye ana usikivu mzuri. Uwekaji na utekelezaji wa mipango mbalimbali katika familia unategemea kusikilizana.

Hebu fikiri baba anataka kujenga wakati mama anataka kununua gari, baba anataka mama asimamie miradi wakati mama anataka kwenda kusoma; ni wazi kuwa hapa kutakuwa na sitofahamu kubwa.
 
Upendo wake haujajengwa kwenye vitu

Mapenzi ya leo kwa kiasi kikubwa hujengwa kwenye vitu na mali. Wengi hupendana kutokana na pesa au mionekano ya nje tu; hili limesababisha wengi kutengana pale vitu hivyo vinapokosekana.

Hakikisha kama unataka kuoana na mtu sahihi unatafuta mtu ambaye upendo wake haujajengwa kwenye vitu vya muda vinavyopita.

“Vitu hutumiwa na watu hupendwa, usitumie watu na kupenda vitu.”
 
Anashukurani

Mtu asiye na shukurani ni mtu asiyefaa kuwepo kwenye ndoa. Watu hawa huwa hawaoni jema wala zuri lolote, wao ni kulalamika na kulaumu tu.

Hakikisha unaoana na mtu mwenye shukurani hata kwa mambo madogo, kwani kwa kufanya hivi mtakuwa na ndoa yenye upendo na kuthaminiana kila mmoja.
 
Tendo la ndoa siyo kipaumbele cha kwanza katika mahusiano

Hili ni tatizo kubwa sana ambalo kwa kiasi kikubwa huharibu mahusiano na ndoa za leo.

Watu wengi hujenga mahusiano yao kwenye tendo la ndoa, jambo linalowafanya wengi kuishia kuzaa nje ya ndoa au hata kutokuwa tayari kuingia kwenye ndoa kwani mambo yote ya ndoa tayari yameshafanywa.

Mtu anayekuthamini hatakutaka kimwili bali atauthamini mwili na utu wako hadi mtakapokuwa kwenye ndoa kamili. Wakati fulani nilisoma mtandaoni kuwa “Vijana wengi wa kiume hawafanyi maamuzi ya kuoa kwa kuwa ngono inapatikana kirahisi”

Kumbuka! Kukutana kimwili siyo tiketi ya kuolewa na mtu; mnaweza kukutana kimwili na bado akakuacha, hivyo kuwa makini.
 
Mkarimu

Mwenzi mkarimu ni bora kwani atakuwa mkarimu kwako, familia yako pamoja na wageni watakaofika nyumbani kwenu.

Unapooana na mwenzi mchoyo ni wazi kuwa ataharibu mahusiano yako na watu; wala hatakuwa tayari kukuhudumia wewe au mtu mwingine kupitia vitu mlivyonavyo.
 
Anakutia moyo

Moja ya jukumu muhimu la mwenzi wa maisha ni kukutia moyo hasa pale unapokutana na changamoto. Hakikisha unaoana na mtu anayeweza kubeba raha na mamumivu yako. Kuna msemo maarufu usemao kuwa “mwanaume anaweza kushinda vita zote ila si ya nyumbani mwake” Jaribu kukumbuka kisa cha Samson na Delila, pamoja na umahiri wa ajabu wa Samson katika vita hakuweza kuishinda vita ya nyumbani mwake iliyoongozwa na mkewe Delila.
 
Anatumia pesa na muda vyema

Mwenzi asiyejua kutumia muda na pesa vyema ni mzigo na hasara kubwa. Ili mtu afanikiwe ni lazima ajifunze umuhimu wa kujali muda pamoja na matumizi mazuri ya pesa.

Hebu fikiri mke anayekaa kwenye televisheni siku nzima au mume anayeshinda kijiweni; niwazi hawa watakuwa masikini na hawataweza kulea familia zao katika malezi bora.

Hakikisha unaoana na mtu anayetunza pesa na muda vyema.
 
Ana ukomavu wa akili

Siyo kila mtu ana akili iliyokomaa kuingia kwenye ndoa. Watu wengine bado ni watoto wadogo ambao hata maaumuzi na matendo yao bado ni ya kitoto.

Ndoa ni swala linalohitaji akili iliyokomaa vyema inayoweza kufanya maamuzi sahihi pamoja na kupambanua jema na baya. Hivyo hakikisha unaoana na mtu mwenye upeo mzuri wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom