Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Takriban wanachama 160,000 wa Conservative walikuwa na fursa ya kupiga kura na katika waliojitokeza ni 87.4%.
Asilimia ya kura kwa Johnson - 66.4% - ilikuwa chini ya aliyojishindia waziri mkuu wa zamani David Cameron mnamo mwaka 2005 aliyejinyakulia 67.6%.
 
Ushindi umepokewaje?
Bi May amempongeza Johnson, na kumauhidi "ushirikiano wake kikamilifu kutoka nafasi ya nyuma".
Rais wa Marekani Donald Trump pia ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akimpongeza Johnson, na kuongeza: "Atakuwa mzuri mno!"
 
Mpango wa kupinga makubaliano ya Brexit wake Johnson utaaminisha waut kupoteza ajira, gharama kubwa madukani na kuhatarisha kuuzwa kwa huduma ya afya ya kitaifa NHS kwa mashirika ya Marekani katika makubaliano na Donald Trump," Kiongozi huyo wa Leba ameendelea kusema.
"Raia wanastahili kuamua nani awe waziri mkuu katika uchaguzi mkuu," ameongeza
 
Changamoto inaanza wakati Johnson apata ushindi
Laura Kuenssberg, Mhariri wa BBC wa kisiasa
Boris Johnson atakuwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Kauli ambayo inaweza kufurahisha au kuogopesha. Kauli ambayo anaeleza kwamba miezi 12 iliyopita hata wafuasi wake sugu hawange weza kuliamini hilo.
 
Changamoto zilizoko ni za kiwango cha kihistoria.
Boris anaipokea serikali ambayo haina uwingi, ilio na siasa ziliyoachanganyika na sera ambayo katika miaka mitatu ijayo Uingereza na Brussels imeshindwa kuitatua.
 
Na yeye ni mwanasiasa, ambaye hata washirika wake wanaoshangazwa na kipaji chake wanakiri hung'ang'ana kutoa maamuzi kwa wepesi.
Mojawapo ya wafuasi wake alitamka leo asubuhi pakisubiriwa tangazo la ushindi: "Changamoto inaanza sasa."
 
Ripoti kutoka Muungano wa kimataifa wa waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi -International Consortium of Investigative Journalists, inasema kuwa makampuni na watu binafsi hutumia taifa la kisiwa lililopo kwenye bahari ya Hindi la Mauritius kuepuka kisheria kulipa kodi kubwa, katika nchi ambazo wanafanyia biashara zao.
 
Mauritius inakanusha kufanya kosa lolote na inasema inatekeleza sheria husika za kimataifa.
Ripoti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia nyaraka 200,000 za siri ambazo zinaonyesha kwa mara ya kwanza ni kwa jinsi gani makampuni ya sheria ya kigeni yalivyosaidia wateja wake wa kigeni kuepuka kulipa mamilioni ya dola ya kodi.
 
Taarifa za rekodi za siri, barua pepe na mafaili, zilizoitwa ufichuzi wa Mauritius, zinafichua utendaji wa kisheria ambao unasaidia kukwepa mapato ya kodi unaofanywa na watu kutoka mataifa ya Afrika , Mashariki ya kati na Asia na kupelekwa mifukoni mwa makampuni ya magharibi , huku Mauritius ikipata sehemu yake.
 
Nyaraka hizo zimetoka katika ofisi ya Mauritius ya kampuni ya sheria yenye makao yake Bermuda inayofahamika kama -Conyers, Dill & Pearman, na nyaraka hizo zinaonyesha taarifa za kipindi cha kuanzia miaka ya 1990 hadi 2017.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…