MFAHAMU MTALAAM WA WANYAMAPORI "DEAN SCHNEIDER", ANAYETIKISA BARA LA AFRIKA KWASASA. . Leo tumuangalie huyu mtaalam wa wanyama anayetikisa bara la Afrika kwenye ufugaji wa wanyamapori wakali. . Dean Shneider anaishi nchini Afrika Kusini kama makazi yake makuu na kipindi cha nyuma alikua anaishi Swaziland na elimu yake ya juu alisema mambo ya uhasibu. Mwaka 2017 aliamua kuacha kazi za taaluma yake na kuanzisha sanctuary yake ya wanyama (Eneo kubwa la kuhifadhi wanyamapori jamii tofauti tofauti), Aliita kwa jina la "HAKUNA MIPAKA" anafuga zaidi Simba, Fisi, Pundamilia na wanyama wengine. Lengo kuu la kufanya hivi ni kuendelea kuwafanya watu kuwa karibu na wanyama hasa hawa wanyama wakali. . Hata hivyo, Dean ameshapata vitasa kibao, bite pamoja na misuko suko mikali kuhusu wanyamapori kama vile kupigwa bite na nyoka na wanyama kumchenjia. Wanyama wa mbugani hawatabiriki ni hatari sana kucheza nao. Siku moja Dean alipoulizwa kwa nini anapenda sana wanyama alisema alivutiwa na mtaalam mmoja aliyeitwa STEVE IRWIN. Je, unamfahamu steve? (Huyu sio yule wa Bongo Movie). . Steve alikua mtaalam sana wa wanyama na alikuwa na Zoo yake iliyotamba sana enzi za miaka ya 2004 nchini Australia, Alikuwa anapenda sana Mamba na kweli Mamba walikuwa wanamheshimu sana, alitengeneza headlines kubwa sana Duniani. Hata hivyo, baada ya kuishi kwa umaarufu kwa muda mrefu, mwaka 2006 Mungu alimchukua katika mazingira yake ya kikazi. Siku ya kifo chake, alikwenda baharini kufanya documentary kama kawaida, lakini alipokuwa huko alikutana na wale samaki wanaitwa sting rays, Bongo tunawaita Taa, hivi haya majina anatunga nani 😀 majina yetu hayana uhalisia kabisaa😀. . Basi taa alimchoma Steve na mkia wake wenye sumu kali sehemu ya moyo na ndio ukawa mwisho wa maisha yake. Kwahiyo Dean akawa ispired na Steve, Na anaonya sana juu ya Raia wanaotaka kucheza na hawa wanyamapori.