Kuwa makini na unywacho;Vinywaji vyenye jamii ya caffeine na pombe, vinaweza kuathiri ubora wa usingizi na hata kuwa macho hadi saa 10 usiku. Vilevile kupata kinywaji cha mvinyo, kunaweza kukufanya ukapata usingizi haraka, lakini ubora wake ukawa shakani.
Zima vitu vyenye mwanga mkali; Epuka kuangalia vitu vyenye mwanga mkali usiku, hasa kompyuta ya kupataka au Laptops na vidonge. Mwanga mkali au kuwa na karibu nalo, una kawaida ya kuchanganya ubongo wa mtu afikiri mapema siku hiyo.
Tulia; Ni vyema kwa mtu kujenga tabia ya kuepuka hali au mambo yanayosumbua anapoenda kulala. Pia, kunapaswa mtu akajenga mazoea ya kila mara kuwa na utulivu, kunywa chai ya viini tiba, kuoga kwa maji ya moto, mazoezi taratibu na kuwa mbali na mingurumo ya simu, kelele na milipuko.
Jenga mazingira sawia; Hakikisha chumba unacholalia kina joto sahihi (si joto sana), giza na kitanda kilichotandikwa na mto unaoleta starehe. Hiyo inachangia kusaidia uzalishaji wa vimelea aina ya melatonin na homoni, zinazochangia kusababisha usingizi.
Kunywa maji ya kutosha; Weka maji ya kunywa. Upungufu wa maji mwilini inachangia kuwepo usingizi wa mang’amung’amu,. Kama mtu hataki kuamka kwa sababu ya kiu ya maji, anywe maji ya kutosha, kukabiliana na hali hiyo.