Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UZAZI WA NDEGE
Kwa kawaida ndege jike hutaga mayai ambayo huangaliwa na kup[atikana kwa kinda. Kabla ya hapo ndege dume na jike hujamiiana ili kurutubisha mayai. Ndege hawanyonyeshi hivyo makinda hukua kwa kuletewa vyakula na wazazi wao wanaovipata kwenye mazingira yanayowazunguka. Idadi ya mayai hutofautiana na aina ya ndege. Kuna wanaotaga mayai mawili kama njiwa na wengini mayai mengi kama mbuni.
 
Baada ya kutaga jike mara nyingi hulazimika kuatamia mayai kwa siku kadhaa kabla ya makinda kuanguliwa. Siku za kuatamia hutofautiana kulingana na aina ya ndege. Wapo wanaoatamia kwa siku 14, 21, 42 au zaidi. Walio wengi huatamia kwa siku 21
 
Wakati wa kuatamia mayai ndege jike hulazimika kukaa kiotani bila ya kula chakula kwa muda Fulani kwa nia ya kuyapa joto mayai. Hali hii hufanya jike kunyonyoka manyoya na hata kukonda. Jike hunyonyoka manyoya sehemu za tumboni ili kuweza kuyapasha joto mayai yake vizuri. Wakati mwingine ndege dume hulazmika kuleta chakula kiotani ili kumlisha jike.
 
Baadhi ya ndege dume husaidia kuatamia mayai jike anapokwenda kujitafuatia chakula. Makinda wanapoanguliwa huwa hawana uwezo wa kuruka kwani mabawa yao hayana manyoya, hivyo hubaki kiotani. Kwa wakati huo jike na dume husaidiana kulinda makinda wao mpaka watakapomudu kuruka na kujitafutia chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…