Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshtuko.
Ok, kumekuwa na ishara kuwa mpenzi wako yuko karibu kukuacha lakini bado unapuuza. Kisha siku moja akakutokea na kukuangalia usoni mwako na kukuambia kuwa wewe na yeye mambo yenu yameisha. Hapo ndipo unakuwa na mshtuko wa mara ya kwanza.
 
Kukataa.
Hii hatua huja baada ya mshtuko wa kuwa umeachwa. Lakini kuna kitu ndani yako ambacho kinakwambia kuwa labda amekasirika tu, atarudi. Unampigia simu, unamtumia sms ukimwomba msamaha huku ukiwa na matumaini ya kuwa atarudiana na wewe.
 
Kujitenga.
Kwa kuwa unaona hataki kujibu meseji zako ama anakataa kuwasiliana na wewe, unaamua kujitenga na dunia. Unafuta namba zake zote za simu. Unajificha nyumbani hutaki mtu yeyote awasiliane na wewe. Unajitenga na uhalisia.
 
Pupa.
Hii hatua huja baada ya kujitenga. Utakuwa umejitenga kwa muda mrefu kisha ghafla unaingiwa na mawazo ya kuwa mwema. Ulipokuwa na yeye katika mahusiano haukuwa unamjali, lakini sahizi unakuja na mbinu mpya za kujaribu juu chini kuhakikisha anakuona kuwa umebadilika na hautakuwa na tabia kama za zamani.
 
Hasira.
Hata baada ya kuonyesha kuwa umebadilika unaona bado mambo hayajabadilika. Hatua hii huja na hasira nyingi za kujutia kwa nini ulikuwa na mahusiano na mtu huyo. Hatua hii unamchukia mtu huyu kiasi cha kuwa unamfananisha na shetani ama adui. Chuki na hasira zisizoisha.
 
Huzuni.
Baada ya hasira, hatua inayokuja unakumbuka kuwa kweli ulikuwa unampenda. Kila mahali ukienda unaona sura yake mbele yako. Unajiona kuwa bila yeye maisha yako hayana maana. Unajiona kuwa hufai katika dunia hii kwa kuwa umemkosa yule mtu ambaye ulikuwa unampenda zaidi hapa ulimwenguni.
 
Unajirudisha nyuma.
Well, ameenda na sioni dalili zozote za yeye kurudiana na mimi. Shida iko wapi? Sijakufa, na kuna wengine wengi ambao wananiona kuwa mimi nafaa. Dunia haitaisha leo. Hii ndio hatua ambao unajikuta unatangamana na wengine ili kujionyesha kuwa kama aliniacha bado naweza kuwa na wengine wengi…lakini mwisho wa siku bado utaona kuwa ulikuwa unajirudia nyuma tu.
 
Kujikubali.
Hii ndio hatua ya mwisho ambayo mtu hupitia akiachwa na mpenzi wake. Nayo ni kujikubali. Maisha yanasonga mbele.
Je sasa hivi uko katika hatua gani? Ama unakumbuka hatua hizi ulipoachwa? Kwa wale ambao bado hawajapatikana kuachwa, fahamu kuwa hizi ndizo hatua ambazo utazipitia.
 
Wewe poti mgumu haya mambo hayakuhusu [emoji16][emoji16][emoji16]

#WaacheKutafutaVisingizio
#WenyeweHawatachapaNje?
#WaacheKujifanyaWatakatifu
#KilaMtunaLwake

Sawa poti, mimi MGUMU kweli kweli. Naongelea wale wenye nia ya dhati kabisa, wale wanakula yamini; kwao, come rain come sun wakishajitosa wamejitosa. Halafu ndio anakuja kusikia sijui “kuchapiwa hakuepukiki”. Please, poti! [emoji16][emoji16]
 
Lakini endapo mwanaume atakuwa haoneshi kumjali, ni vigumu sana mke kuendelea kuwa muaminifu na katika mazingira hayo ndiyo unaweza kusikia, mke katembea na shemi yake au mtu mwingine. Hata hivyo, najua wapo wanaojiuliza sababu hasa za mke kufikia katua ya kuchepukia kwa rafiki wa mume wake. Nimechunguza na kubaii baadi ya sababu kama zifuatazo hapa chini;
 
Moja; endapo utakuwa umeingia kwenye ndoa na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku. Kwa mfano, endapo umeoa lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’ mkeo, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mkeo atahisi yeye ni mtu sahihi kwake
 
Mbili; Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahsi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?
Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.
 
Tatu;Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.
Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mpenzi wako baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo. Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.
Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mpenzi wako aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukua mpenzi wako kwenye gari kumrudisha nyumbani. Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mpenzi wako kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.
 
Nne; unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakuchukulia mpenzi wako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.
Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wapenzi wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa wapenzi wao au wapenzi wa mashoga zao.
 
Tano; Endapo utagundua mpenzi wako katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.
Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliye naye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonesha mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.
 

Mwenyekiti naona unaweka mambo sawa lakini wewe unaonaje kwa mtazamo wako ni kweli ???

Kuchapiwa hakuepukiki
 
Hapo nakubaliana na wewe kabisa bro tena asilimia 200% mfumo dume umekosea na ni unafiki, Mimi concern yangu ni wale ambao hawachapi lakini wanachapiwa hawa ndiyo concern yangu ipo sana kwao

Wale Wanafiki achana nao ?
Kulingana na Masoud Kipanya hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja tu maishani mwake. Unaichukuliaje kauli hii? Kwa hali ya sasa hasa kwenu vijana inawezekana kweli kijana aoe na atulie kabisa kabisa na mke wake asichape nje no matter what? Naamini inawezekana lakini ni asilimia ndogo sana labda 1%.

Hawa wanaochapa nje hawana haki ya kulalamika wakichapiwa. Cha ajabu wachapa nje ndiyo wanaongoza kwa kuwa na wivu wa kupindukia. Hata hawa wanaochinja wachumba na wake zao kila leo ukichunguza vizuri utakuta wana michepuko kibao huko nje.

Ila kama umejitoa kabisa kabisa na uko faithful 100% ukichapiwa bila shaka utaumia sana. Na una haki ya kufanya hivyo !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…