Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"


Masud kipanya ulikuwa ni mtazamo wake, kama inawezekana kwa watu kama kina lebron James, billget wenye pesa na ushawishi itashindikana vipi kwangu mimi wa mbagala ambaye sina pesa wala ushawishi

Dhana ya masoud ukiifafanua zaidi kama anataka kutuambia kwamba wanawake ni kwa ajili ya starehe tu, of which kwa Dunia ya leo haiwezekani

Wachapaji nje wengine ndiyo mpaka wanaua wanaowatuhumu hawa ni wanafiki sana, kama utakuwepo moto nafikiri watakuwa kuni

Kujitoa inawezekana lakini una chance kubwa ya kupata maumivu ukidondokea sehemu ambayo si salama
 

Yaani poti niache kuwa nasema #KuchapiwaHakuepukiki# kisa nakatisha tamaa waoaji?

Nikibadilisha na kuanza kusema #KuchapaNjeHakuepukiki# itapunguza makali kidogo na kuwafanya waoaji wasijisikie vibaya?

[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Sikujua kama nilikuwa nakwaza watu poti. Ningekuwa nimeshaacha zamani...
 

[emoji16][emoji16][emoji16]... Unaongezea idadi ya wagumu poti! Ila haya mambo ni magumu sana, tena kwa pande zote mbili. Ukiingia yakakushinda tafuta uchochoro ulale mbele.
 
Mimi nipo kwenye hiyo 1% aisee.
Ugumu wangu umestiki kwa mmoja 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ugomvi baina ya wapenzi katika mahusiano ni kitu cha kawaida kutokana na watu hao wawili kutoka katika malezi na mazingira tofauti ya ukuaji toka wakiwa wadogo hadi watu wazima.
Wawili hao wanapoaanza kujenga mahusiano na kukaa pamoja kama familia,kuna vitu kadhaa ambavyo kila mmoja wao huvitazama tofauti na hivyo kuleta migongano.
 
Naunga mkono hoja, hii kauli kama una mtu lazima uwaze mara mbili mbili kwamba ina ukweli kweli??

 
Migongano ambayo inaweza ikarekebishika kama wenza hao watamua kuifanyia kazi na kuelewana.
Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano ndani ya mahusiano ya mke na mme na hapa tunaeleza sababu kuu ambazo kwa kawaida hutokea karibu katika kila mahusiano
 
Wivu Na Kukosa Kujiamini
Wivu unatokana na jinsi ambavyo mpenzi mmoja anavyohusiana na watu wengine wa jinsia tofauti. Inaweza ikawa marafiki,wafanyakazi wenza au wapenzi wa zamani. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba wivu unasababisha ugomvi katika mahusiano mengi.
 
Kunatakiwa kuweka mipaka ya kutosha na iliyo wazi ili kujenga uaminifu kwa mpenzi wako na kumpa kujiamini. Mpenzi ambaye hajiamini ni tatizo kubwa kwani uwezekano wa kuanzisha ugomvi ni mkubwa.Hivyo ni vizuri ukamjengea mweza wako katika mapenzi kujiamini kwa kuwa mwaminifu.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]... Unaongezea idadi ya wagumu poti! Ila haya mambo ni magumu sana, tena kwa pande zote mbili. Ukiingia yakakushinda tafuta uchochoro ulale mbele.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mawasiliano Finyu
Mawasiliano yanapovunjika katika mahusiano ugomvi ni kitu cha kawaida kutokea.
Mawasiliano ya kawaida kati ya wapenzi husaidia sana kutoa wasiwasi wa nyendo za mwenza wako. Huleta amani na kujenga uaminifu kwa mpenzi kwako.
 
Kuzungumza juu ya mipango yako ya mendeleo kama ujenzi au biashara ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuvifanya vinginevyo utajenga wasiwasi kwa mweza wako na itasababisha ugomvi wa mara kwa mara.
Kuwa muwazi kwa mipango ya maendeleo binafsi,ya familia yako na ndugu.
Utafiti unaonyesha kuwa wapenzi wanaoongea na kusikilizana mara kwa mara hawagombani mara nyingi kama wale wasio na mawasiliano ya kutosha.
 
Masuala Ya Fedha
Japokuwa fedha si msingi wa mapenzi,lakini ni kitu ambacho kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo wapenzi katika mahusiano au ndoa hugombana sana juu yake.
 
Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine siyo,huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya wapenzi hasa wanawake hawataki kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wanaume.
Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya wanaume,na wakati ungine toka kwa wanawake. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na sharehe nyingine kwa wanaume na baadhi ya wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.
 
Masuala Ya Familia
Familia ya nani ianze kwanza na ipi ifuate ni tatizo kubwa katika mahusiano. Upendeleo wa upande mmoja ambao kwa asili huwa unatokea tu ni chanzo cha ugomvi ndani ya nyumba.
Mitazamo tofauti kati ya mmojawapo katika wapenzi na familia ya mwenza wake husababisha kutoelewana kwa wapenzi hao ndani ya nyumba.
Mbaya sana inakuja pale wanandugu wanapoingilia mambo ya ndani ya nyumba yenu. Wazazi wa kike na mawifi mfano, wamejulikana kusababisha matatizo mengi kwenye familia za watoto na kaka zao.
Kuepukana na hili ni muhimu kwa wapenzi ndani ya nyumba kuweka mipaka kwa ndugu ambayo haitaathiri uhusiano nao kama ndugu.
Pia ni muhimu kwa wenza hao kuweka mikakati ya pamoja juu ya kuhusiana nakusaidia ndugu toka katika familia zao mbili.
 
Suala La Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao wana uhitaji tofauti.
Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.
Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.
 
Vipaumbele Katika Maisha
Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.
Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…