Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

images.jpg
 
Njia ya kisasa ya kufanya utafiti; utafiti wa simba sio kazi nyepesi hata kidogo, imegubikwa na hatari nyingi, hasara nyingi na pia changamoto nyingi sana. Hata hivyo pamoja na hayo yote lazima tujifunze njia nzuri za kuishi na wanyama hawa kwa kufanya utafiti za kina na wa kutosha. Utafiti wa simba katika eneo hili la Hwange ulifanyika kwa kuwafunga simba cola. Kola au Collar ni vifaa vinavyofungwa shingoni mwa mnyama yeyote kwa ajili ya kumfuatilia, kujua alipo na umbali anaotembea.
 
Umuhimu wa kuwafunga wanyama kola, wanyama kama simba ni wanyama ambao wanaweza kusambabisha madhara kwa watu, hasa jamii ya wafugaji, hivyo kwa kuwa na njia ya kuwafunga kola ni rahisi kujua walipo na pia kujua wanakoelekea. Njia hii ni nzuri sana kwasababu inawasaidia wahifadhi na watafiti wa masuala ya uhifadhi kubuni mbinu bora za uhifadhi wa wanyamapori kama simba.
 
Ufungaji wa kola kwa simba kwa ajili ya kumfuatilia ni kazi nzito ambayo inahitaji watu wenye uelewa na watalaamu wa kufanya hivyo. Sio kila mtu anaweza kumfunga simba kola, kuna watalamu wamesomea mambo hayo, wanajua namna ya kushika simba, namna ya kupima dawa ambayo inampa usingizi na sehemu za kumpiga dawa hiyo. Kitendo cha kumshika simba kinaitwa kudati, mnamdati simba kwa kumpiga kwa kutumia bunduki ambazo zina sindano zenye dawa ya usingizi sehemu husika akisha lala hapo ndio tayari kwa kumfunga kola, kuchukua sampuli kama vile damu na kinyesi kwa ajili ya kwenda kupima maabara.
 
Back
Top Bottom