Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Hatari ya kupata magonjwa kutoka kwa simba kipindi cha kumfanyia utafiti, hasa kumfunga kola, kuchukua sampuli kama damu na kinyesi. Simba wana minyoo mibaya sana inayoitwa “Taenia spp”, pale unapogusana au kumshika simba kuna mayai ya miyoo hiyo hatari ambayo usipokuwa mwangalifu unaweza kuambukizwa kwa kula na minyoo hiyo kuingia ndani ya mwili wako na kuanza kukusumbua na kusababisha hata kifo. Hivyo katika protokali za utafiti wa simba huwa wanazingatia sana jambo hilo, unawza kuvaa gloves, na baada ya kufanya shughuli zote, ni inashauriwa kunawa mikono kwa maji mengi na sabuni.