Simba ni mnyama anayejulikana zaidi na kupendwa na watu wengi zaidi, watu wengi wanamchukulia simba kama alama ya ushujaa, ujasiri, nguvu na mamlaka, picha nyingi sana, vinyago na mabango mengi sana yana nembo ya simba. Filamu nyingi sana, nyumba na hata kwenye sehemu muhimu sana zina nembo ya simba. Simba amekuwa akihusishwa sehemu nyingi kama alama ya uwezo na uongozi, vitabu vingi sana vina picha za simba kuliko wanyama wowote wale. Mwandishi anasema katika jiji la London kuna picha, nembo na mapambo mengi yenye nembo ya simba kuliko simba walio hai katika Afrika Magharibi.