Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mie nadhani hii inatokana na ukweli kuwa chakula ndio kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu ajisikie vizuri katika ngazi yeyote ile ya maisha. Ukila vizuri unajisikia vizuri na afya tele, hata kama ni mara moja kwa mwaka. Lakini kuna tatizo kwenye kupenda sana kula, hasa vile vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu, utaishia kuongeza uzito ambao una madhara makubwa kwenye afya yako
 
Lakini leo hatuzungumzii kula vizuri, wala kunenepa, bali tunaangalia njia ya kula chakula vizuri na kuwa na uhakika wa kutoongeza kalori (carolies) nyingi mwilini, hivyo kukufanya uwe na afya zaidi. Na mada yetu inahusu zaidi kwenye kula viporo - iwe wali maharage, tambi au vyakula vingine vingi.
 
65977142_2490857794522998_8315645953732802724_n.jpg
 
ANGALIZO: Ukimaliza kusoma hii habari, kimbilia kiporo chako cha wali na maharage na ukile hadi ukinai, maana ni habari njema kwa wale wanaopenda kula bila kuongeza kilo kwenye miili yao. Kuwa makini tu jinsi ya kupasha moto.
Kula vyakula vilivyotoka kuandaliwa ni salama na afya zaidi, hii haina ulazima wa ufafanuzi. Lakini kuna jamii ya vyakula ambavyo ni vizuri zaidi kula vikiwa kama viporo. Aina mojawapo muhimu sana la hivi vyakula ni kundi la vyakula vya wanga (carbohydrates).
 
Tunakula vyakula vya wanga mara nyingi sana kwenye milo yetu ya kila siku. Ukila vyakula vya jamii ya wanga unaongeza kiwango cha sukari kwa kasi sana kwenye damu, wakati wa mmeng'enyo, hivyo hulazimu mwili kufanya kazi ya ziada ya kutoa kimeng'enyo cha insulin kinachofanya kazi ya kupunguza sukari kwenye damu. Hii kupanda na kushuka kwa damu kwa kasi husababisha chakula kusagwa haraka sana na unaweza kusikia njaa muda mfupi baada ya kula. Hii pia ni jibu mojawapo kwanini unasikia usingizi ukiwa umetoka kula chakula cha wanga - sukari na mwili kufanya kazi kwa nguvu - hukufanya kuwa na uchovu na uvivu.
 
Lakini, leo nna habari tofauti. Imefanyika utafiti na inaonyesha kuwa kuna utofauti wa umeng'enyaji kati ya wanga uliopikwa (wa mtoto), uliopoa na ule uliopoa na kupashwa moto. Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na kuripotiwa na BBC hapa. Utafiti unaonyesha kuwa kiwango cha mmeng'enyo na sukari kwenye damu kinapungua kama wanga ikipikwa na kuliwa kama kiporo (baridi), lakini hupunguza zaidi kiwango cha sukari kwa asililia 50% kama ikiwa kiporo na kupashwa moto.
 
Hii inamaanisha nini kwako wewe mlaji?

Utafiti huu unatoa ufafanuzi mzuri juu ya vyakula tunavyokula. Kutokana na matokeo haya, ni vizuri zaidi kula na kushiba kiporo cha jamii ya wanga sababu hakitokufanya uongezeke uzito kama utakapokula chakula cha kawaida. Hii ni kwa sababu nusu ya chakula unachokula ndio kinachotumika kukupa karoli mwilini na kilichobaki huishia kutoka kama makapi.
 
Watu wengi sana wanapenda kupunguza uzito bila kuvuruga kula, hii inawezekana kama utafanya mazoezi magumu na ya muda mrefu. Lakini kwa kupata matokeo mazuri zaidi, kupunguza kula vyakula visivyo na afya ni kitu muhimu zaidi kuliko hata mazoezi. Nasema hivi sababu chakula ndio kinachokufanya uongezeke uzito, lakini si swala la kujinyima kula, ni swala la kujua jinsi ya kula vyakula visivyokufanya unenepe. Vyakula vya kuzuia ni chumvi, sukari, na mafuta yasiyo na afya kama yalivyoelezewa hapa. Lakini leo unaongeza kiporo kwenye orodha ya vyakula vya kula bila kuwa na wasiwasi wa kunenepa.
 
Unaweza kuwa na swali, je kwanini ukila kiporo huwa nahisi kuvimbiwa na tumbo kujaa? Jibu ni rahisi, na sababu pekee ni kuwa unakosea kupasha moto kiporo chako, na jibu liko hapa chini. Lakini kwanza tuangalie jinsi ya kuhifadhi kiporo.
 
Hivyo basi, ili kulinda chakula muda mrefu na kuepukana na madhara ya kuingiwa na vijidudu vinavyoweza kuleta sumu, weka chakula kwenye jokofu mara tu baada ya kumaliza kula. Vyakula vingi huharibika haraka na kuingiwa na wadudu mara tu vikishapoa, hasa vyakula vyenye protini ambavyo huharibika haraka sana vikihifadhiwa vibaya. Ni vizuri kulinda afya yako kwa kuhakikisha chakula kimehifadhiwa vizuri ili kuweza kuliwa wakati kinapohitajika.
 
Back
Top Bottom