Asante bro. Nikiri tu kuwa hiyo siyo kauli yangu. Nadhani ni kauli ya askari mmoja wa Kifaransa aliyekuwa anapigana vita visivyo na maana kule Algeria. Alishangaa kwamba hata baada ya ushindi kupatikana yeye hakuona faida yo yote ya vita vile.
Na ukiangalia vizuri katika maisha yetu. Kinafsiya tunapigana vita vingi vya kisaikolojia, kiroho na hata kimwili lakini ukichunguza vizuri utagundua kwamba mara nyingi hakuna faida yo yote ambayo tunaipata katika mapigano haya na mara nyingi tunaishia kujiumiza tu.
Ni vizuri angalau kuwa na utambuzi wa kung'amua vita tunavyostahili kupigana katika maisha yetu kwa sababu kwa kufanya hivyo tunajipa amani, ridhiko na kumakinikia zaidi mambo ya muhimu kwetu kwa wakati huu na ujao...
Naipenda falsafa hii [emoji1545][emoji1545]