Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maji ya mchele yana vitamini kama vile B1, C, E, pamoja na madini, ambayo yanaweza kupunguza matobo katika ngozi, kukaza ngozi, kupunguza mistari ya uzee na pia kuang’aza ngozi yako.
 
Namna Ya Kutengeneza Maji Ya Mchele



safisha mchele kwa kutumia maji ili kuondoa uchafu au uchafu wowote. Weka mchele katika bakuli miminia maji. loweka mchele wako kwa dakika 30, kisha toa mchele katika maji hayo na mimina maji yako katika chombo safi na maji yako ya mchele yatakuwa tayari kwa matumizi
 
Namna Ya Kutumia Maji Haya Kung’aza na Kusafisha Uso

Jinyunyuzie maji ya mchele kidogo katika uso wako na taratibu massage uso wako kwa dakika moja, baada ya hapo osha uso wako kama kawaida na utaanza kuona matokeo katika ngozi yako, fanya hivi kabla ya kwenda kuoga. unaweza kuhifadhi maji yako katika kikopo chenye mfuniko, unaweza kuyatumia kwa siku 5 baada ya siku hizo tengeneza mengine.
 
Broccoli ni aina ya mbogamboga ambayo inataka kufanana sana na kabeji, lakini yenyewe majani yake huwa na muonekano wa kijani sana tofauti na ilivyo kwenye kabeji.Vile vile ni tofauti na Cauliflower, cauliflower ni nyeupe Wakati broccoli ni ya kijani.
 
Mara nyingi mbogamboga hii hutumiwa sana na wahindi na hata kupatikana imekuwa ikipatikana sana kwenye masoko yanayotembelewa sana na watu wa jamii hiyo. Kwa Dar es salaam Inapatikana Sokoni kisutu na Mwenge.
 
Mfumo wa Neva: Inasaidia kufanya mfumo mzima wa neva kufanya kazi inavyotakiwa na kufanya ubongo kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa ina madini ijulikanayo kama potasiamu (potassium), na kisha misuli kuwa na nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…