Hali iliyotukia nchini Indonesia mwaka wa 1997 ni mfano mmoja unaoonyesha jinsi moto unavyoweza kusababisha hasara kubwa sana. Mwaka huo mioto iliteketeza vichaka nchini humo, iliharibu sana ardhi, ikadhuru afya, na kusababisha hasara ya kiuchumi. Na moshi mbaya sana wa mioto hiyo ulisambaa katika nchi jirani—jumla ya nchi nane—ukawaathiri watu wapatao milioni 75. Ripoti zinaonyesha kwamba watu milioni 20 waliugua ugonjwa wa pumu, ugonjwa wa kuvimba mapafu, magonjwa ya moyo, ya macho, na ya ngozi.